Wizara ya Mambo ya Nje ya Russia ilitangaza Ijumaa jioni kwamba Moscow imewawekea vikwazo raia 500 wa Marekani, akiwemo rais wa zamani wa nchi hiyo, Barack Obama.
Wizara ya Mambo ya Nje ya Russia imetangaza kuwa Moscow itazuia kuingia nchini humo Wamarekani 500, akiwemo rais wa zamani wa Marekani, Barack Obama, ikiwa ni jibu kwa vikwazo vya mara kwa mara vya Marekani.
Ujumbe uliochapishwa kwenye tovuti ya Wizara ya Mambo ya Nje ya Russia umesema: “Ili kukabiliana na vikwazo vya kimfumo vya utawala wa Joe Biden dhidi ya Russia, ambavyo vimewekwa katika kalibu ya mpango wa Washington wa kusababisha hasara kubwa zaidi kwa Russia na kuwaathiri maafisa na raia wa kawaida, Shirikisho la Urusi limewazuia Wamarekani 500 kuingia katika nchi hii.”
Wizara ya Mambo ya Nje ya Rusia imesisitiza kuwa umefika wakati kwa Washington kujifunza kwamba shambulio hata la chuki dhidi ya Russia halitapita hivihivi bila kupewa jibu kali.
Wizara ya Mambo ya Nje ya Russia pia imetangaza kwamba Moscow imekataa ombi la hivi karibuni la Marekani la kuwaruhusu maafisa wa ubalozi wake kukutana na ripota wa Wall Street Journal, Ivan Gershkevich, ambaye alikamatwa mwezi Machi kwa tuhuma za kufanya ujasusi.
Russia imetangazwa kuwa hatua hiyo imechukuliwa kama jibu kwa uamuzi wa mwezi uliopita wa Marekani wa kukataa kutoa viza kwa vyombo vya habari vya Russia vilivyotakiwa kusafiri kwenda Umoja wa Mataifa na Waziri wa Mambo ya Nje, Sergey Lavrov.