Sababu kuu ya umma kukaa kimya kunako Palestina inahitaji utambuzi:Hujjatul Islam Ustad Syed Jawad Naqvi

Hujjatul Islam Ustad Syed Jawad Naqvi

(Principal Jamia Orwatul Wuthqa – Lahore)
imetolewa: Masjid Baitul ul Ateeq
Lahore – Pakistan

Hotuba ya Ijumaa – 21st June, 2024

 

Hotuba ya 1: Maana ya Wilaya katika fasihi ya Kiarabu na Qur’an
Hotuba ya 2: Sababu kuu ya umma kukaa kimya kunako Palestina inahitaji utambuzi
Maisha ya kijamii ndio msingi wa maisha ya mwanadamu ambapo vipengele vingine vya maisha hujengeka na kukua kupitia maisha haya ya kijamii. Uwanja tawala w2a maisha ya kijamii upo katika maisha ya kisiasa. Usaliti na udanganyifu sio siasa kitu ambacho kinatazamiwa kwa wanasiasa. Siasa ina maana ya kusimamia na kuongoza maisha, nchi, nyumba na uchumi n.k. kwa kua mwanadamu ana utashi na hiari, anahitaji sera ya kusimamia na kuendesha maisha yake ambayo ni dini kwa kufuata maelekezo aliyoyatuma yakiwa ni mwongozo.
Katika maisha ya kijamii mfumo ambao kwao mfumo mzima wa maisha ya kijamii utatengenezwa ni siasa ambao Allah hakuwaachia wanadamu wajitengenezee. Namna ambavyo Allah aliumba viumbe na kuvipatia kila kitu kimsingi. Namna hiyo pia ametengeneza mpango, usimamizi na siasa kwa ajili ya maisha ya kijamii. Cheo cha juu cha siasa ya kijamii ni Wilaya ambapo mtu anatakiwa kuishi chini ya Wilayat. Mfumo ni Wilaya tu kama mwanadamu atapata kwa kuzingatia sera za Mwenyezi Mungu itakuwa ni Wilaya ya Mwenyezi Mungu vinginevyo itakuwa ni Wilaya ya Taghoot. Mwenyezi Mungu hakumpa Wilaya Taghoot bali watu ndio huamua kuwafuata. Watu wanapomchagua Walii, wanachagua Taghoot lakini Mwenyezi Mungu anapomteua Walii ni kwa mujibu wa Wilaya.
Kuna mengi yamesemwa, yameandikwa kuhusu Wilaya lakini hakuna anayejua kuhusu maana ya Wilaya. Katika mfumo huu wa Wilayat Mwenyezi Mungu amezungumza kuhusu Taqwa ambayo ina maana kwamba unapaswa kupata Taqwa katika Wilaya. Ukipata Taqwa katika nyanja ya maisha ya kijamii na kisiasa basi maisha yote katika nyanja zote yatakuwa salama.
In Surah Maida, verse no 57
يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا لَا تَتَّخِذُوا الَّذِينَ اتَّخَذُوا دِينَكُمْ هُزُوًا وَلَعِبًا مِنَ الَّذِينَ أُوتُوا الْكِتَابَ مِنْ قَبْلِكُمْ وَالْكُفَّارَ أَوْلِيَاءَ ۚ وَاتَّقُوا اللَّهَ إِنْ كُنْتُمْ مُؤْمِنِينَ {57}
Enyi mlio amini! Msiwafanye marafiki wale walio ifanyia kejeli na mchezo Dini yenu miongoni mwa walio pewa Kitabu kabla yenu, na makafiri wengine. Na mcheni Mwenyezi Mungu kama nyinyi ni wenye kuamini.
Msifanye Walii kuwa kundi fulani lililoelezwa hapo juu na mpate Taqwa ikiwa nyinyi ni Waumini. Msipopata Taqwa katika Wilaya basi nyinyi si waumini. Maisha ya mwanadamu yanakuwa salama kupitia mfumo wa Wilaya.
Katika Aya ya 54 ya Surah Maida
يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا مَنْ يَرْتَدَّ مِنْكُمْ عَنْ دِينِهِ فَسَوْفَ يَأْتِي اللَّهُ بِقَوْمٍ يُحِبُّهُمْ وَيُحِبُّونَهُ أَذِلَّةٍ عَلَى الْمُؤْمِنِينَ أَعِزَّةٍ عَلَى الْكَافِرِينَ يُجَاهِدُونَ فِي سَبِيلِ اللَّهِ وَلَا يَخَافُونَ لَوْمَةَ لَائِمٍ ۚ ذَٰلِكَ فَضْلُ اللَّهِ يُؤْتِيهِ مَنْ يَشَاءُ ۚ وَاللَّهُ وَاسِعٌ عَلِيمٌ {54}
Enyi mlio amini! Atakaye iacha miongoni mwenu Dini yake, basi Mwenyezi Mungu atakuja leta watu anao wapenda nao wanampenda, wanyenyekevu kwa Waumini na wenye nguvu juu ya makafiri, wanapigania Jihadi katika Njia ya Mwenyezi Mungu, wala hawaogopi lawama ya anaye laumu. Hiyo ndiyo fadhila ya Mwenyezi Mungu, humpa amtakaye. Na Mwenyezi Mungu ni Mkunjufu na Mwenye kujua.
Iwapo nyinyi waumini mkiuacha mfumo wa Mwenyezi Mungu na kwenda kwenye mfumo usiokuwa wa Mwenyezi Mungu basi mtaruhusiwa kuondoka lakini Mwenyezi Mungu atauweka badala yenu umma mwingine unaompenda Mwenyezi Mungu na Mwenyezi Mungu anawapenda. Sifa yao ya pili ni kuwa wakali kwa makafiri na wapole kwa waumini. Sifa ya tatu ni kwamba watajitahidi na kupambana katika njia ya Mwenyezi Mungu maana yake ni kutumia uwezo wao wote katika njia ya Mwenyezi Mungu. Sio kwamba watatumia mali zao kwa burudani na furaha ya kibinafsi. Uwezo waliopewa na Mwenyezi Mungu watautoa na kuutumia katika njia ya Mwenyezi Mungu. Sifa ya nne ya jumuiya hii itakuwa kwamba hawataogopa wakosoaji na dhihaka. Hii ni sifa kubwa kwa sababu nyakati fulani mwanadamu anaweza kuvumilia mateso ya kimwili lakini hawezi kuvumilia mateso ya kisaikolojia. Hii ni fadhila ya Mwenyezi waliyopewa amtakaye Mwenyezi Mungu. Sifa hizi nne hazipewi kwa wale wanaokanusha au wanaogeuka nyuma kutoka kwenye mifumo ya kiungu, lakini sifa hizi zipo katika wale wanaokuja mahali pao.
Katika aya inayofuata, Wilaya wamepewa watu hawa wanaokuja mahali pa Murtad. Wana sifa za kupata Wilaya.
إِنَّمَا وَلِيُّكُمُ اللَّهُ وَرَسُولُهُ وَالَّذِينَ آمَنُوا الَّذِينَ يُقِيمُونَ الصَّلَاةَ وَيُؤْتُونَ الزَّكَاةَ وَهُمْ رَاكِعُونَ {55}
Hakika rafiki yenu mlinzi ni Mwenyezi Mungu na Mtume wake na walio amini, ambao hushika Sala na hutoa Zaka nao wananyenyekea.
Mfumo maalum wa Wilayat umetunzwa kwa ajili ya watu maalum wale tu wanaostahiki na sifa hizi nne. Baada ya kutaja sifa hizi nne katika Aya ya 54 na kisha katika Aya ya 55 Wilayat imetajwa kuwa inahusishwa na sifa hizi nne. Tumesikiliza Wilaya kutoka kwa wasemaji jambo ambalo ni kwa ladha yao na ambalo limesababisha kuwatenga mbali Mashia kutoka kwenye Wilaya hii halisi.
Katika aya hii rejea inaelekezwa kwa Imam Ali (a) ambaye alitoa Zaka katika hali ya kurukuu katika Swala. Hii ina maana Imamu Hassan (a), Imamu Husein (a) na wengineo hawakufanya hivi, kwa hiyo wao si Mawalii? Utathibitishaje Wilaya yao? Aya hii inawasilisha sera. Kwamba walii ni Mwenyezi Mungu, Mtume wake, Waumini wanao simamisha Swala na kutoa Zaka katika hali ya Rukuu kwa mujibu wa Qur’an. Hii inajumuisha Maimamu wote. Sehemu hii inahitaji ufafanuzi zaidi ambao tunaweza kuufanya baadaye katika mihadhara yetu ya Tafsiri.
Katka Aya ya 56
وَمَنْ يَتَوَلَّ اللَّهَ وَرَسُولَهُ وَالَّذِينَ آمَنُوا فَإِنَّ حِزْبَ اللَّهِ هُمُ الْغَالِبُونَ {56}
Na atakaye fanya urafiki na Mwenyezi Mungu na Mtume wake na walio amini, basi hakika kundi la Mwenyezi Mungu ndilo lenye kushinda.
Wale wanaokubali Wilaya ni Hizbullah. Hizbullah kwa mujibu wa Quran ni wale walio na sifa nne zilizotajwa katika aya ya 54. Pamoja na sifa nne wanaikubali Wilaya takatifu na Hizbullah ni washindi na wanatawala.
Katika Aya ya 57 mpangilio wa Taqwa unakuja
يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا لَا تَتَّخِذُوا الَّذِينَ اتَّخَذُوا دِينَكُمْ هُزُوًا وَلَعِبًا مِنَ الَّذِينَ أُوتُوا الْكِتَابَ مِنْ قَبْلِكُمْ وَالْكُفَّارَ أَوْلِيَاءَ ۚ وَاتَّقُوا اللَّهَ إِنْ كُنْتُمْ مُؤْمِنِينَ {57}
Enyi mlio amini! Msiwafanye marafiki wale walio ifanyia kejeli na mchezo Dini yenu miongoni mwa walio pewa Kitabu kabla yenu, na makafiri wengine. Na mcheni Mwenyezi Mungu kama nyinyi ni wenye kuamini.

Aya inasema ni nani msimchukue kama Walii. Hao ndio wale ambao walioifanyia mzaha Dini yenu, wakaifanya uwanja wa michezo sawa sawa wawe ni katika watu wa vitabu vilivyo tangulia au vya sasa na makafiri. Hapa ndipo mnaamrishwa kuchukua Taqwa. Kama utapata Taqwa kwenye Wilaya hiyo ina maana ya kukubali mfumo wa Wilaya ya kiungu tu kisha Maisha yako yote na Nyanja zote za Maisha huwa salama.
Wilayat ni nini? Vikundi vyote vimejadili kwa kina kuhusu Wilaya na vitabu vilivyopo juu ya mada hii ya Wilaya ni vingi sana kiasi kwamba unahitaji zaidi ya miaka mia moja ya maisha ili kusoma vitabu vyote. Lakini ni nini Wilaya hii katika Quran? Quran imetumia lugha ya kawaida ya Kiarabu kueleza maana zake, lakini haipati lugha ya sayansi yoyote maalum iliyopo wakati huo au ijayo. Hii ina maana kwamba tusijaribu kuelewa istilahi za Qur’an kupitia sayansi nyinginezo kama vile Tasawwuf n.k. Theolojia, Fiqh, Ugnostiki ni sayansi ambazo zilikuja baadae kutoka kwenye Quran kwa hiyo haziwezi kuwa chanzo cha kuelewa istilahi za Qur’ani.
Quran imetumia Kiarabu kilichokuwepo kabla ya kushuka kwa Quran. Hivyo ili kuelewa neno Wilayat, Walii inabidi tuone maana yake katika lugha ya Kiarabu na kisha tuone kama Quran imetumia katika muktadha huo huo. Tunaposoma tafsiri ya Quran tunapaswa kuwa waangalifu kwani tafsiri hizo pia zinafanywa kwa kuzingatia mrengo ya umadhehebu. Wanajaribu kutoa madhehebu kutoka kwenye Qur’an au kuanzisha madhehebu katika Quran. Kama vile Taqwa inavyotafsiriwa na kila mtu kuwa ni kumuogopa Mwenyezi Mungu au kujiepusha na mambo fulani. Kwa Wilayat pia imetafsiriwa kama marafiki au wale walio karibu na Mwenyezi Mungu.
Wilayat ni neno la Kiarabu na daima kuna mzizi wa neno Wa La Ya. Maana halisi ya asili si ukaribu, urafiki au ulezi. Istilahi hizo zilizaliwa katika utamaduni wa Kiarabu na mtindo wa maisha. Waarabu wanapoweka kitanzi juu ya Ngamia au tandiko juu ya farasi huumiza mgongo wa farasi. Farasi na ngamia ni wanyama wenye thamani kwa Waarabu. Migongo ya ngamia na farasi haswa wakati wa kiangazi hujeruhiwa kwa sababu ya tandiko. Kwa hiyo, huweka kitambaa laini kati ya tandiko na mgongo wa mnyama. Nguo hii inaitwa na Waarabu kama Walaya. Inamaanisha kwamba hupaswi kuweka tandiko moja kwa moja juu ya mgogo wa ngamia bali badala yake uweke kitambaa hiki kwanza. Hakuna kitu kinachokuja kati ya mgongo na tandiko. Walaya ni kile kitambaa ambacho huwekwa moja kwa moja kwenye mgongo wa mnyama bila ya kuwa na kitu chochote katikati. Kutokana na hili neno Walaya lilianza kutumika kwa mambo mengine pia.
Mvua inaponyesha jangwani, kwa vile jangwa ni kavu mvua ya kwanza inaponyesha maji yote humezwa na ardhi. Mvua hii haina faida yoyote kwa mwanadamu. Kisha mvua inayofuata inayokuja bila pengo Waarabu wangetamani na kungoja, kwani maji yatajaa kwenye visima na sehemu zingine. Mvua ya kwanza inaitwa Wasmiya na mvua ya pili ambayo maji yake huwa muhimu huitwa Walaya maana yake mara baada ya Wasmiya. Baada ya hapo Waarabu walianza kutumia neno Walaya kwa kitu chochote kinachokuja bila pengo baada ya kitu cha kwanza na kutimiza mahitaji ambayo hayajatimizwa na cha kwanza.
Kwa hivyo, maana ya kimsingi ya Walaya ilikuwa ni kitu chochote kinachokuja na kufunika, kuchukua kitu na kutimiza mahitaji ya kitu hicho. Taratibu maana hii ilianza kutumika kwa watu fulani pia. Walii alikuwa ni mtu ambaye atakuja mbele zaidi kutimiza haja ya mtu yeyote bila wakati wowote kupita baina yao au mara moja. Kama kwa watoto wadogo yule ambaye ni yule mlezi ambaye huwalea bila ya kuwa na mtu yeyote kati yao, au moja kwa moja kivuli chake kinakuwa juu ya watoto kama ndege wanavyofanya. Mwanadamu akifanya hivi basi yeye ni Walya. Jambo la kwanza linalokuja kuelewa kitu na kutimiza mahitaji .
Neno Wali lilitumika kabla ya Quran na Quran ilitumia neno hili kwa maana yake iliyokuwepo. Mwanadamu anaishi katika jamii na ana mahitaji na tegemezi katika kila nyanja ya maisha. Hakuna binadamu anayejitegemea. Mfumo ambao Mwenyezi Mungu ameuweka kwa ajili ya kiumbe hiki chenye kuhitaji ili kutimiza mahitaji yake ya kijamii, binafsi, ya kifamilia, ya ndani, ya nje, mahitaji ya kiroho ya muumini bila ya yeyote kati yake, moja kwa moja hii ni Wilayat. Mfumo huu umetengenezwa kwa ajili ya kulinda maisha ya mwanadamu pale ambapo Mwenyezi Mungu ameyafahamu maisha ya mwanadamu. Hii ni Wilayat.
Kwanza Mwenyezi Mungu ameeleza kuwa amekufahamu kutoka pande zote maana yake Mwenyezi Mungu amepanga kwa ajili ya mahitaji yote ya mwanadamu. Hii ina maana kwamba mamlaka yote ya mwanadamu yako kwa Mwenyezi Mungu na hadhi hiyo hiyo wanapewa Mitume wa Mwenyezi Mungu. Hii ina maana bila pengo mtu mwenye mamlaka na kuitawala jamii ni Mtume. Kisha wale wanaoswali, kutoa Zaka na kurukuu pia wanapewa Wilaya. Ufahamu huu ni kusaidia na kutimiza mahitaji. Maana ya mbali sana ambayo haihusiani na Wilaya ni urafiki. Tuna marafiki wengi sana ambao hawaji kwa aya kutimiza hitaji letu au tunafanya kitu. Katika Kiarabu Hubb inatumika kwa maana ya urafiki. Walii ndiye anayechukua mamlaka ya jamii na kuyaendesha kwa mujibu wa mfumo wa Mwenyezi Mungu na hivyo kutimiza haja. Ufahamu na mamlaka vipo ili kutimiza mahitaji fulani na kupewa ulinzi. Kama kitambaa kilichowekwa juu mgongo wa farasi ni kwa ajili ya kulinda mgongo kutokana na majeraha. Maana hiyo hiyo inatumiwa na Quran. Wilaya ina maana ya ufahamu wa maisha ya mwanadamu ambayo Mwenyezi Mungu anayo mamlaka na kisha kwa wengine ambao Mwenyezi Mungu amewapa mamlaka hayo. Wilaya hii haikomei tu kwa Maasum. Mifumo yote ya ulimwengu inaendeshwa kwenye Wilaya kama vile watoto, mke, familia, Khums, maiti zote zina mutawalli.
Wilaya kwa uhalisia ni mfumo, ngome inayofahamu maisha yote ya mwanadamu. Hapa Mwenyezi Mungu anasema kwanza ni nani walii wenu, kisha ni nani msifanywe kuwa walii kama wale wanaoifanyia mzaha dini yenu. Hapa tunatafsiri kama urafiki. Haimaanishi kwamba haupaswi kusalimiana nao. Unapaswa kuwa na urafiki na wanadamu wote lakini huwezi kumfanya kila mtu kuwa Walii. Hii ni Taqwa ambapo inabidi uonyeshe usikivu na kulinda mfumo na usije kuruhusu mtu mwingine yeyote kuwa Walii.
Hii ni wiki ya Wilaya na tutaendelea na mjadala huu.
HOTUBA YA PILI
Kizazi cha sasa kinatoa uthibitisho wa moja kwa moja kwamba hakuna ubinadamu. Dini bila Taqwa haitoi faida yoyote na uthibitisho wa hili ni Palestina. Kundi moja linafanya ubabe, ushenzi na kupumzika na wengine wote wako kimya. Fitra ya Binadamu hujibu inapoona matukio kama haya na ukatili hata kwa wanyama. Katika wanyama pia unapoona mbwa anashambulia mtoto na paka humuokoa mtoto. Hii ni silika ya mnyama, lakini anapopoteza Taqwa anakuwa duni kuliko wanyama.
Ndani ya Pakistan hapo awali kwa ajili ya tembo kelele kubwa ya kimataifa ilitolewa. Hivi majuzi huko Sindh mguu wa ngamia aliye hai ulikatwa na taifa zima linaandamana. Gavana wa Sindh alisema atatuma ngamia apelekwe Dubai kwa matibabu. Yote haya ni unafiki. Mnaonesha huruma nyingi kwa ngamia lakini hamtoi na hamna machozi kwa ajili ya kuwalilia watu elfu arobaini, watoto, Waislamu na kwenye njia sahihi huko Palestina. Huu ni unyama.
Kila utakatifu umekiukwa huko Gaza. Waislamu ndio wamefanya hivi zaidi. Imam e Kaaba wakati wa Hijja ametoa hotuba ya kusema na akawaombea Wapalestina kwamba Mwenyezi Mungu awape maji na chakula ambacho kinaonekana kuwa ni neema kubwa aliyowafanyia Wapalestina. Katika hali hii ya kutokuwa na wasiwasi na kuguswa ni muhimu zaidi kujua jinsi Waislamu hawa walivyo kuwa wa aibu, wasio na hisia. Kwa nini Hamas inapigana na Israel inaua tunaijua sisi, lakini kwanini Waislamu wako kimya ni kutokana na ugonjwa mkubwa unaohitaji kugundulika. Wakati Imamu Husein (a) alipoanza harakati yake ya kupinga , watu wengi walijaribu kumkataza. Muhammad Ibn Hanafiya alianza kutoka Madina hadi Makka ili kumsimamisha na kumzuia Imam, na alishikilia utawala wa ngamia wa Imam Husein (a) huko Makka bila kumruhusu kuendelea. Imamu Husein (a) alitoa wosia wa maandishi kwa Ibn Hanafiya. Katika ujumbe huu aliandika kwamba ninakwenda kufanya matengenezo ya Ummah ambao una maana kwamba kulikuwa na ufisadi katika Umma. Alikaa Makka kwa muda wa miezi minne na kueleza hali hiyo kila siku lakini hawakusogea na hakuna hata mtu mmoja aliyeongeza idadi na kujiunga naye. Utovu wa hisia ulikuwa kwenye kilele na hivyo Imam (a.s.) akasema kwamba Ummah huu unahitaji marekebisho. Ikiwa Ummah utaharibika basi katika kila zama atazaliwa dhalimu. Kuwepo kwa Israel, kuimarishwa, kushambulia Palestina, kuharibu Gaza ni ishara ya ufisadi katika Umma. Sote tunawajibika na tunafikiri kwamba kwa vile hatuwezi kufanya lolote tunanyamaza. Una simu ya mkononi na unaweza kuposti angalau ujumbe mmoja kila siku kwenye Facebook. Hata wakifunga ukurasa wako, tengeneza mwingine na kufunga kwao kunamaanisha kuwa ni mzuri na wenye taathira. Unaweza kuendelea na maandamano yako endelevu.
Tuna uchungu sana kwa ngamia, na jana mtu mmoja alichomwa moto kwa kuichafua Quran, sasa kwa nini mmekaa kimya kuhusu Palestina. Ulimwengu mzima unangoja kama watazamaji kuona Palestina ikiharibiwa. Hali imebadilika na Hizbullah wameweka mikono yao kwenye shingo ya Israel sasa. Baraza la mawaziri la vita la Israeli lilipigana kwa mikono ndani na Netanyahu alimaliza baraza la mawaziri la vita. Kuna kesi katika mahakama za kimataifa dhidi ya Israel. Israel inasalia leo kutokana na watawala wa Kiarabu. Waarabu wanadhani kwamba ikiwa Hamas watabaki basi utawala wao utakuwa umekwisha. Wajibu wa Ummah unasubiri ambao kila mtu anatakiwa kuutekeleza.

Previous Post
Next Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *