Faraan: Cristiano Ronaldo alijiunga na klabu ya Saudi Al-Nasr kwa mkataba wa euro milioni 200.
Ijapokuwa kuajiriwa kwa wachezaji wa mpira kutoka nchi tofauti ni jambo la kawaida, lakini kuajiriwa kwa Ronaldo katika klabu ya al-Nasr ya Saudi Arabia kuna uchambuzi na uvumi wakivyake kulingana na macho ya watu wa Saudia na bila shaka maoni ya umma nje ya nchi hii;
Katika uvumi, baadhi ya watu wa Saudia wanaamini kuwa baada ya michuano ya Kombe la Dunia kufanyika nchini Qatar na nchi hii kuwa kitovu cha tahadhari ya kimataifa, wivu wa bin Salman dhidi ya nchi hii ulizidi hivybasi kujaribu kuvutia hisia za walimwengu kwa kumsajili mchezaji huyo mwenye wafuasi wengi zaidi duniani.
Baada ya miaka mitatu na nusu ya kujaribu kuitenga Qatar na wakati huo huo kupindua serikali ya nchi hii, Saudi Arabia ilibusu mkono wa Amiri wa Qatar na kupungukiwa na masharti 11 yaliyowekwa kwa ajili ya kufufua uhusiano pamoja na nchi hii, ingawaje bado haina mtazamo chanya wa nchi hii na katika Kila hali inajaribu kufidia kushindwa katika uzio wa miaka mitatu na nusu uliowekwa kwa Qatar; Jambo la kufurahisha na la kuzingatiwa ni michuano ya Kombe la Dunia iiyofayika nchini Qatar;
ni kua amir wa nchi hii alijaribu kwa kutumia mbinu zenye busara ya hali ya juu kulazimisha mila za Kiislamu na za Kiarabu kwa watu waliotoka maeneo tofauti tofauti ulimwenguni wakati wa michuano hiyo.
Alifanya hivi kwa Kuwasilisha picha zenye kuafiki maombi ya jamii ya Kiislamu, kuzuia uhuru wa mashoga nchini Qatar, na kusaidia katika uungaji mkono wa umma kwa kadhia ya Palestina, na hatimaye kuufunika mwili wa Lionel Messi kwa abaya ya Kiarabu ikiwa ni miongoni mwa hatua hizo.
Baadhi ya watu wengine wa Saudia wanaamini kuwa Bin Salman anajaribu kuboresha na kujenga upya sura yake ya kimataifa kwa kumwalika Ronaldo kujiunga na Klabu ya Al-Nasr.
Mauaji ya Khashoggi kwa amri ya moja kwa moja ya Bin Salman, mauaji ya halaiki, ambayo ya hivi karibuni zaidi yalikuwa miezi michache iliyopita, na kunyongwa kwa watu 81 kwa wakati mmoja bila kupitia michakato ya kisheria, na… inahusu Bin. Salman kama mtawala mkali anayepinga haki za binadamu na uhuru wa umma. Haiwezekani kusahaulika au kurekebishwa na hatua hizo.
Nukta moja wakati wa michezo ya Kombe la Dunia ilitajwa mara kwa mara na watu wa Saudi, na inawezekanaje bin Salman akasafiri hadi Qatar na kuanza kutazama michezo, lakini wapinzani ambao walikuwa wakipinga na kukosoa sera zake kuhusiana na uhusiano na Qatar bado mtuhumiwa wa kukosoa sera zake kukaa gerezani
Ben Salman; Ni Bin Salman, na bila shaka, idadi isiyohesabika ya wafungwa wa dhamiri, takwimu zilizotangazwa za wale ambao wamenyongwa na wale wanaongoja kunyongwa, n.k., ni uthibitisho wa mtazamo huu dhidi ya haki zake za kibinadamu.
Je, unaweza kufikiria Bin Salmani, ambaye, pamoja na kuendeleza uasherati na ufisadi katika ardhi ya wahyi, na pia kwa jina la kutoa uhuru wa kijamii, atasimamisha umwagaji damu na uharibifu wa uhuru wa umma nchini Saudi Arabia? Jibu la swali hili linaweza kupokelewa katika siku chache zijazo; Kwa mujibu wa habari, karibu watu 50 watanyongwa nchini Saudi Arabia wakati wa Krismasi.