Safari ya Netanyahu nchini Ujerumani huku maandamano ya Wazayuni yakiendelea

Serikali ya Ujerumani ilitangaza kuwa kansela wa nchi hiyo atakuwa mwenyeji wa waziri mkuu wa Israel katika mkutano wa “chakula cha mchana” mjini Berlin Alhamisi hii.

Afisa wa Ujerumani alitangaza mpango wa Waziri Mkuu Olaf Schultz kwa ajili ya mkutano wa pande mbili na Benjamin Netanyahu huko mjini Berlin.

Vyanzo vya habari kutoka Berlin, mji mkuu wa Ujerumani, vilitoa maelezo kuhusu mpango wa safari wa Benjamin Netanyahu ambaye ni Waziri Mkuu wa utawala wa Kizayuni kuelekea kwenye nchi hiyo ya Ulaya.

Kulingana na ripoti ya Reuters, mmoja wa wasemaji wa serikali ya Ujerumani alitangaza kwamba kansela wa nchi hii atakuwa mwenyeji wa Netanyahu katika mkutano wa “chakula cha mchana” siku ya Alhamisi.

Kulingana na ripoti hiyo, Shultz na Netanyahu watazungumzia masuala ya pande mbili za Berlin na Tel Aviv, masuala ya usalama wa kikanda na wa kimataifa, na kuhusu mpango wa baraza la mawaziri la Netanyahu wa kurekebisha muundo wa mfumo wa mahakama wa Israel.

Msemaji wa serikali ya Ujerumani aliongeza kuhusu mkutano wa Olaf Schultz na Benjamin Netanyahu: “Waziri Mkuu anatazamiwa kuhudhuria katika mkutano huu.”

Taarifa ya mamlaka ya Ujerumani kuhusu ziara inayokuja ya Waziri Mkuu wa utawala wa Kizayuni mjini Berlin ilitekelezwa katika hali ambayo maandamano dhidi ya Netanyahu yanaendelea katika Palestina inayokaliwa kwa mabavu.

Kushadidi maandamano katika Palestina inayokaliwa kwa mabavu na matamshi ya viongozi wa Marekani wanaokosoa mpango wa baraza la mawaziri la Netanyahu wa kurekebisha mfumo wa mahakama wa utawala wa Kizayuni kumezusha mvutano katika uhusiano kati ya Tel Aviv na Washington.

Hivi karibuni, afisa wa ngazi ya juu wa Kizayuni aliye karibu na Netanyahu aliitaja serikali ya Joe Biden kuwa ina jukumu la kufadhili maandamano ya nchi nzima katika Palestina inayokaliwa kwa mabavu.

Previous Post
Next Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *