Safari ya Rais Assad UAE: Syria kurejea tena katika Jumuiya ya Arab League

Rais Bashar al-Assad wa Syria jana aliwasili katika nchi ya Umoja wa Falme za Kiarabu na kulakiwa rasmi na Rais Mohammed bin Zayed al-Nahyan ikiwa ni ishara ya wazi ya kuhuishwa uhusiano wa Syria na mataifa ya Kiarabu ya Ghuba ya Uajemi baada ya zaiidi ya muongo mmoja.

Hii ni ziara ya pili ya Rais wa Syria katika Ghuba ya Uajemi tangu kutokea kwa tetemeko la ardhi nchini Syria. Rais wa Syria anafanya ziara katika Umoja wa Falme za Kiarabu baada ya ziara ya hivi karibuni katika nchi ya Oman na ziara yake ya juzi nchini Russia.

Ziara hii mpya ya Rais wa Syria katika Umoja wa Falme za Kiarabu ni hatua moja zaidi ya ‘kurudi’ Damascus kwenye “Jumuiya ya Nchi za Kiarabu ” ameandika, Anwar Gargash, mshauri wa kwanza wa Rais wa Imarati Mohamed bin Zayed, kwenye ukurasa wake wa Twitter.

Taarifa zaidi zinasema kuwa, ziara hiyo inaonekana kuwa sherehe zaidi ikilinganishwa na ziara ya huko nyuma alipokwenda imarati mwaka jana ambayo ilikuwa ya kwanza katika taifa la Kiarabu tokea kuanza vita vya wenyewe kwa wenyewe mwaka 2011 vilivyochochewa na madola ya Magharibi na baadhi ya mataifa ya Kiarabu.

Katika kipindi hicho mataifa ya Ghuba ukiwemo Umoja wa Falme za Kiarabu yaliwaunga mkono makundi ya kigaidi ili kumuondoa madarakani Rais Bashal al-Assad. Hata hivyo baada ya zaidi ya muongo mmoja inaonekana kuwa, mataifa ya Kiarabuu yamelazimika kurejesha uhusiano na Syria baada ya kushindwa kufikia malengo yao.

Akiwa nchini Imarati, Rais Assad amekutana na kufanya mazungumzo na Rais Sheikh Mohammed bin Zayed al-Nahyan na kupewa heshima ya saluti wakati ujumbe wake ulipokuwa ukiingia kwenye makazi ya kifalme. Aidha Ndege ya Rais Assad ilipokelewa na ndege za kivita za Imarati.

Previous Post
Next Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *