Hujjatul Islam Ustad Syed Jawad Naqvi
(Principal Jamia Orwatul Wuthqa – Lahore)
imetolewa: Masjid Baitul ul Ateeq
Lahore – Pakistan
Hotuba ya Ijumaa – 3 May, 2024
Hotuba ya1: Matokeo ya kumiliki Imani, Taqwa, Tawakkal
Hotuba ya 2: Salamu kwa wanafunzi wa vyuo vikuu vya Marekani na fedheha kwa Waislamu
Katika maisha ya kila siku tunaamini na kutegemea mambo mbalimbali, kama vile unapoajiri wafanyakazi fulani, au kufanya biashara na mtu kuna kuaminiana. Mkulima anapopanda mbegu, ana Tawakkal kwamba mbegu hii itaota ikiwa kuna udongo na nyenzo nyinginezo. Lakini ni kiasi gani kilimo hicho kinategemea nyenzo na ni kiasi gani kiko mikononi mwa Mwenyezi Mungu. Mwalimu wetu angesema ikiwa tajiri atasema unasoma nami nitakulipia gharama zako zote, tunafurahi na kuaminiwa, lakini ahadi hiyo hiyo imetolewa na Mwenyezi Mungu lakini hatuna hata 1% ya Tawakkal juu ya Mwenyezi Mungu. Tuna Tawakkal kwa jamaa na wengineo lakini sio kwa Mwenyezi Mungu.
Kuna siri ambayo wale wanaostahiki wataelewa. Kila mtu hachukui muongozo wa sehemu yake ambayo iko pamoja na Quran kwa sababu hakuna mahali. Quran imeeleza siri fulani na katika baadhi ya sura kuhusiana na Tawakkal. Katika Surah Talaq, inaanza na suala la talaka.
يَا أَيُّهَا النَّبِيُّ إِذَا طَلَّقْتُمُ النِّسَاءَ فَطَلِّقُوهُنَّ لِعِدَّتِهِنَّ وَأَحْصُوا الْعِدَّةَ ۖ وَاتَّقُوا اللَّهَ رَبَّكُمْ ۖ لَا تُخْرِجُوهُنَّ مِنْ بُيُوتِهِنَّ وَلَا يَخْرُجْنَ إِلَّا أَنْ يَأْتِينَ بِفَاحِشَةٍ مُبَيِّنَةٍ ۚ وَتِلْكَ حُدُودُ اللَّهِ ۚ وَمَنْ يَتَعَدَّ حُدُودَ اللَّهِ فَقَدْ ظَلَمَ نَفْسَهُ ۚ لَا تَدْرِي لَعَلَّ اللَّهَ يُحْدِثُ بَعْدَ ذَٰلِكَ أَمْرًا {1}
Ewe Nabii! Mtakapo wapa talaka wanawake, basi wapeni talaka katika wakati wa eda zao. Na fanyeni hisabu ya eda. Na mcheni Mwenyezi Mungu, Mola wenu Mlezi. Msiwatoe katika nyumba zao, wala wasitoke wenyewe, ila wakifanya jambo la uchafu ulio wazi. Hiyo ndiyo mipaka ya Mwenyezi Mungu, msiikiuke. Na mwenye kuikiuka mipaka ya Mwenyezi Mungu, basi amejidhulumu nafsi yake. Hujui; labda Mwenyezi Mungu ataleta jambo jengine baada ya haya. (1)
فَإِذَا بَلَغْنَ أَجَلَهُنَّ فَأَمْسِكُوهُنَّ بِمَعْرُوفٍ أَوْ فَارِقُوهُنَّ بِمَعْرُوفٍ وَأَشْهِدُوا ذَوَيْ عَدْلٍ مِنْكُمْ وَأَقِيمُوا الشَّهَادَةَ لِلَّهِ ۚ ذَٰلِكُمْ يُوعَظُ بِهِ مَنْ كَانَ يُؤْمِنُ بِاللَّهِ وَالْيَوْمِ الْآخِرِ ۚ وَمَنْ يَتَّقِ اللَّهَ يَجْعَلْ لَهُ مَخْرَجًا {2}
Basi wanapo fikia muda wao, ima warejeeni muwaweke kwa wema, au farikianeni nao kwa wema. Na mshuhudishe mashahidi wawili waadilifu miongoni mwenu. Na simamisheni ushahidi kwa ajili ya Mwenyezi Mungu. Hivyo ndivyo anavyo agizwa anaye muamini Mwenyezi Mungu na Siku ya Mwisho. Na anaye mcha Mwenyezi Mungu humtengezea njia ya kutokea. (2)
وَيَرْزُقْهُ مِنْ حَيْثُ لَا يَحْتَسِبُ ۚ وَمَنْ يَتَوَكَّلْ عَلَى اللَّهِ فَهُوَ حَسْبُهُ ۚ إِنَّ اللَّهَ بَالِغُ أَمْرِهِ ۚ قَدْ جَعَلَ اللَّهُ لِكُلِّ شَيْءٍ قَدْرًا {3}
Na humruzuku kwa jiha asiyo tazamia. Na anaye mtegemea Mwenyezi Mungu Yeye humtosha. Hakika Mwenyezi Mungu anatimiza amri yake. Mwenyezi Mungu kajaalia kila kitu na kipimo chake. (3)
Unapompa talaka mwanamke muache nyumbani kwako amalize Eda yake usimtoe nyumbani, fanya tabia hii nzuri. Kisha siri hasa ya kitendo hiki inatajwa katika Aya inayofuata.
Pindi tulipo muuliza rafiki ya Imam Khomeini kunako siri iliyopo nyuma ya mafanikio yake, alitusomea Aya hii na kusema hii ndio ilikuwa siri ya mafanikio yake ambayo Imam Khomeini alifunzwa na mwalimu wake. Watu hawakuwa tayari kwa ajili ya mapinduzi pamoja na maulama ambao walikuwa wakimsifia Shah kuwa alikuwa shia. Maulama walimuwekea vikwazo Imam Khomeini kwanza, kisha Shah na alifukuzwa nchini na kisha baadaye ndio Imam alipofaulu. Tulimuuliza rafiki yake moja kwa moja na alijibu kwa kusema pindi Imam(r.a) alipoelezea magumu yake kwa mwalimu wake, alipata jibu hili katika Aya ya 2 na 3.
مَنْ كَانَ يُؤْمِنُ بِاللَّهِ وَالْيَوْمِ الْآخِرِ ۚ وَمَنْ يَتَّقِ اللَّهَ يَجْعَلْ لَهُ مَخْرَجًا {2}
anaye muamini Mwenyezi Mungu na Siku ya Mwisho. Na anaye mcha Mwenyezi Mungu humtengezea njia ya kutokea
وَيَرْزُقْهُ مِنْ حَيْثُ لَا يَحْتَسِبُ ۚ وَمَنْ يَتَوَكَّلْ عَلَى اللَّهِ فَهُوَ حَسْبُهُ ۚ إِنَّ اللَّهَ بَالِغُ أَمْرِهِ ۚ قَدْ جَعَلَ اللَّهُ لِكُلِّ شَيْءٍ قَدْرًا {3}
Na humruzuku kwa jiha asiyo tazamia. Na anaye mtegemea Mwenyezi Mungu Yeye humtosha. Hakika Mwenyezi Mungu anatimiza amri yake. Mwenyezi Mungu kajaalia kila kitu na kipimo chake.
Yeyote mwenye kuipata Taqwa, basi Mwenyezi Mungu
Whoever acquires Taqwa Allah establishes a way out from him and provides him with provisions from place, sources where he never even thought about. And whoever does Tawakkal on Allah, Allah suffices for him and Allah makes his affair reach success. Allah has made a system for everything.
Mwenye kupata Taqwa basi Allah humtengenezea njia ya kutoka kwake na humruzuku riziki kutoka mahala, na vyanzo ambavyo hakuwahi kuvifikiria hata kidogo. Na yeyote anaye mtegemea Mwenyezi Mungu, basi Mwenyezi Mungu humtosheleza na Mwenyezi Mungu hulifanya jambo lake kufikia mafanikio. Mwenyezi Mungu ameweka utaratibu na mfumo kwa ajili ya kila kitu.
Hii ni aya ya siri ambapo Mwenyezi Mungu anasema yeyote ambaye ana Tawakkal juu ya Mwenyezi Mungu, Mwenyezi Mungu humtengenezea njia ya riziki yake kutoka katika chanzo ambacho kamwe hajakifikiria. Riziki maana yake ni utoaji wowote ambao ni muhimu kwa ajili ya kuendelea kuwepo kwa kitu ambacho hufika kwa wakati maalum na kipimo kinachohitajika. Ikiwa una imani (Imaan), Taqwa na Tawakkul basi matokeo fulani yapo; Moja ni Mwenyezi Mungu humruzuku, humwezesha riziki kutoka katika vyanzo visivyojulikana na Mwenyezi Mungu humjaalia kujitegemea kutoka katika kuwategemea wengine kama vile Mwenyezi Mungu alivyokuwa ni mwenye kujitosheleza. Lakini Mwenyezi Mungu ameweka mfumo kwa kila jambo na anafanya kwa mujibu wa mfumo huo.
Katika maisha yetu sisi ni tegemezi katika mambo yetu kwa mambo mbalimbali, watu, mafisadi, washirika, polisi, Hakimu na hii ndio Tawakkul. Kama ukiiacha Tawakkul na kutomwamini mtu yeyote basi hutaweza kufanya lolote. Tawakkal hii ni yenye kutegemena lakini Mwenyezi Mungu anasema mfumo huu ni wangu, wewe fanya sehemu yako na kinachobaki niachie mimi.
Kwa ujumla hatuziamini ahadi za Mwenyezi Mungu. Mwalimu wetu huyo huyo angesema katika matukio fulani maalum kwamba Mwenyezi Mungu hukuweka kwenye mitihani basi njia wewe unapaswa kumchunguza Mwenyezi Mungu pia kama anatimiza ahadi au la. Kama ahadi hii iliyopo katika Surah Talaq ambapo mwenye imani, Taqwa na Tawakkul basi Mwenyezi Mungu humruzuku wakati kila inapoonekana kufungwa kila kitu. Hatuko tayari hata kuchunguza. Katika biashara tunafanya mikataba ya majaribio lakini kwa Mwenyezi Mungu hatuko tayari hata kujaribu kana kwamba tuna hakika kwamba haya yote ni mazungumzo ya bure katika Quran. Tumemuacha Mwenyezi Mungu na kuchukua njia za riziki kuwa kama mfumo wa elimu unaotolewa na wazazi na hatuna imani na Mwenyezi Mungu. Leo hii nchi yetu iko kwenye matatizo na wanajaribu kutafuta njia za kutoka na hatimaye wakapata njia (Makhraj) kutoka IMF yaani kwa kuchukua mikopo zaidi. Hatujaijaribu hata mara moja njia iliyoonyeshwa na Mwenyezi Mungu. Watu wote hawa wa kidemokrasia wanafanya ukafiri kwa kutokuwa na Tawakkulul juu ya Mwenyezi Mungu. Ikiwa hutatii, basi hii ni aina moja ya Kufuru. Kama hushukuru kutokana na yale ambayo Allah kakupa kwa kutumia katika njia ambazo Allah kakuonyesha, basi hii ni aina ya pili ya kufuru na aina ya tatu ni kufuru dhidi ya Tawakkul. Allah ametengeneza mfumo wa imamat ambao unauamini lakini hauna imani na Tawakkul juu yake. Tuna Tawakkul na waharibifu, wazinzi lakini na sio na Mwenyezi Mungu. Basi kuna ujumbe gani tunao upata.
Leo tunaishi katika ulimwengu wa mseto ambapo tumechanganya aina mbili tofauti za vitu. Leo kuna magari ya mseto ambayo hufanya kazi kwa petroli na betri. Tunasema kwamba nchini Pakistani kuna demokrasia ya mseto ambapo watu wanapiga kura na vyombo vya dola pia zinawekwa nguvu zao. Utamaduni wetu ni mseto, ambapo sisi ni Waislamu, Wahindu na WaMagharibi pia. Kitu ambacho ni cha mseto zaidi ni dini yetu. Tumechukua baadhi ya vitu kutoka katika Quran, na pia tumechukua vitu fulani kutoka kwa Ahlulbayt (a) , kisha kutoka kwenye utamaduni. Dini tuliyonayo katika maisha yetu ni sawa na chumvi kwenye mkate. Katika kilo moja ya unga wa ngano, unaweka chumvi kidogo. Unga wa ngano sio dini chumvi kidogo ndio inawakilisha dini, wengine wana shinikizo la damu kwa hiyo wanaweka chumvi kwenye dini tu wakati wa Muharram au Ramadhani. Katika ndoa zetu Nikah pekee ndiyo inatokana na dini.
Lau tungekuwa na dini ya kipekee basi mfumo wetu wote ungetokana na dini, katiba yetu ingekuwa Quran, kiongozi wetu angekuwa Walii na ilani yetu ingekuwa Uimamu. Bado hatujafanya Tawakkul kwa Mwenyezi Mungu. Je, kuna tatizo katika kuwa na Tawakkul kwa Mwenyezi Mungu? Ikiwa utafanya Tawakkul kwa Mwenyezi Mungu basi Mwenyezi Mungu amekuwekea njia zote. Dini hii ya mseto ni udanganyifu tu ambapo pepo inaundwa kwa utaratibu na wasemaji. Tumelipa pesa kwa wabunifu kwa ajili ya kubuni pepo. Mwisho wa mfumo wa mseto ni moto wa Jahannam.
Tawakkul ni siri nzito ya ndani ambayo Allah ameieleza na wale ambao wamefaulu katika dini ni kutokana na siri hizi. Inabidi tuweze kuzitwaa hizi ahadi za Mwenyezi Mungu na ili tuweze kupata mafanikio.
HOTUBA YA 2
Maisha bila Taqwa hubadilika na mabaya zaidi ya Wanyama ambao mifano yao inaonekana katika historia kama ilivyoelezwa na Qur’an na Ushahidi mkubwa juu ya hili ni kizazi cha leo kinachomfanya vitendo vya kinyama. Leo hii kila kinacho tokea Gaza na Palestina. Kila mtu yupo kimya juu ya udhalilishaji na unyama kwa ujumla. Lakini bado ubinadamu unaweza kuonekana katika baadhi ya maeneo yasiyo tarajjiwa. Kwa mfano Amerika Wanafunzi wa vyuo wamepaza sauti kiasi kwamba imefikia hatua mfumo wa Amerika kutumia nguvu, na jeshi dhidi yao ijapokuwa wengi wao sio Waislamu. Wameweka mahema na kambi za kupinga na kuimba nyimbo za kudai uhuru wa Palestina na baadhi ya vyuo huko California waliwaadhibu vikali na kuwaumiza Wanafunzi na kukamata baadhi yao. Biden anasema: sisi sio madhalimu lakini kuhusu Palestina hatutamruhusu yeyote kupaza sauti. Hawakutegemea lakini limetokea ndani ya nyumba ya Shetani. Hawa mabinti hawana hijabu lakini wamewakilisha ujumbe na kuvaa uhusika kuliko mwanamke wa Kiislamu aliyevaa hijabu. Wanaendelea na mapambano ndani na nje ya vyuo vikuu kitu ambacho kimewapa Wapalestina faraja na utulivu. Tukitazama vyuo. Ikiwa tutatazama vyuo vikuu nchini Pakistan na mataifa mengine ya Kiislamu kama Indonesia, Malaysia. Miaka ya 100 ya Madrassa ya kidini haijapaza sauti lakini vyuo vikuu hivi sio Madrassa lakini wamejifunza ubinadamu na kutoa changamoto kwa serikali yao kwamba mnafanya hivi huko Palestina na ni uhalifu. 100 mamia ya maelfu wameuawa kishahidi huko Palestina na sasa ona kile ambacho vyombo vya habari vimesema. Katika mpaka karibu na Jordan Magharibi mtoto mmoja aliuawa na majeshi ya Israel na sasa wamesema kuwa huo ni uhalifu wa kivita, lakini watoto 1000 waliouawa Palestina hawawaoni.
Waziri wetu wa mambo ya nje ametemelea OIC na kuisifia kwa sababu OIC inaongozwa na Saudi Arabia. OIC haijafanya kitu hadi tarehe ya leo kwa ajili ya Waislamu. Kisha unamuona huyu kinyonga Erdogan na wanyama hawa wote kuwa ni kielelezo cha ubinadamu
Kisha unaona kinyonga huyu Erdogan na wanyama hawa wote ni alama za sifa za kibinadamu. Watu wa aina hiyo hubadilisha rangi popote pale walipo chini ya aina ya watu waliopo huko. Erdogan ni shujaa wa kuigwa fulani nchini Pakistan. Katika habari za Dawn news leo imetajwa kuwa Uturuki imekata uhusiano wote wa kibiashara na Israel. Uturuki ni mfano wa kuigwa kwa Nasibi ( wanawafanyia uadui Ahlul Bayt) na Takfiri ( wenye kukufurisha watu). Iran imeweka vikwazo kwa Uingereza na Marekani jambo ambalo ingawa ni ishara lakini linahitaji ujasiri. Kulingana na Al Jazeera, Uturuki imevunja uhusiano na Israel kutokana na dhuluma huko Gaza na haitashughulika na kuwa na uhusiano na Israel hadi watakapo maliza na kufikia mwisho wa vita huko Gaza. Hii ina maana kwamba Uturuki ilikuwa ikifanya biashara na Israel hadi leo na msaada mkubwa umetolewa na Uturuki. Kwanini vikwazo hivi vimewekwa na Israel? Hii ni kwa sababu waziri wa mambo ya nje wa Israel aliwashawishi Waturuki kuamka dhidi ya Erdogan kwa sababu ni dikteta ambaye anakandamiza maslahi ya kiuchumi ya watu na nchi. Uturuki ilikuwa inachukua mafuta bure kutoka Azarbaijan na kuyasafirisha kwenda kwenye jeshi la anga la Israel takriban ndege 300 hadi 400 kwa siku kwa kutumia jeshi la Israel. Kuna bidhaa za aina 54 ambazo Uturuki ilikuwa ikisafirisha kwenda Israel. Biashara katika ya Uturuki na Israel ilikuwa ni billioni 6 USD kabla ya kuanza kwa vita vya Gaza, na baada ya vita kuanza ilifikia billioni 9 USD ambayo Uturuki ilikuwa ikisafirisha. Uturuki imetoa kambi ya jeshi la anga na kambi ya mafunzo kwa Israel. Erdogan hakukata mahusiano ya kidiplomasia na Israel kama alivyokuwa pia hajafunga ubalozi wa Israel. Azarbaijan imetoa mipaka yote inayo shirikiana na Iran kwa Israel kupitia Uturuki ambapo Israel ana kambi. Katibu wetu wa wizara ya mambo ya nje anatoa taarifa kila siku kwamba hatutoi kambi yeyote kwa Amerika. Kwa hivyo kwa nini wanasema hivi kila siku? Amerika inataka kuweka kambi kuizunguka Irani na hii wanataka sana baada ya shambulio la Irani kwa Israeli. Sasa wakati IMF inapo idhinisha mikopo ya dola bilioni 8 mara moja kwa Pakistan si chakula cha mchana cha bure. Hii ndiyo hali ya Waislamu na tabia yao ya uhusika. Kilichoanza katika chuo kikuu cha Amerika kilitarajiwa, kwa sababu damu ya mashahidi hawa ilitarajiwa kuonyesha rangi. Qatar inatoa maagizo kwa Hamas kuondoka Qatar ikiwa hawawezi kuwaachilia wafungwa na Jordan inawaalika Hamas kuja Jordan jambo ambalo ni baya zaidi kwani wao (Jordan) ni washirika wakubwa wa Israel. Katibu wa zamani wa Amerika ametangaza kuwa nchi sita za Kiarabu zimehakikisha na kutoa dhamana ya ulinzi wa Israeli. Nchi hizo ni Uturuki, Jordan, Saudi, UAE zimechukua jukumu kubwa katika kuilinda Israel. Kila damu ya mtoto wa Kipalestina ina uhusika wa mikono ya Erdogan na Wapakistan wanapaswa kujua hili. Tunawasalimu watoto hawa na wanafunzi wa chuo kikuu cha Marekani ambao hawana uhusiano na Wapalestina lakini wanapaza sauti zao, lakini Waislamu ambao ndio wenye uhusiano wako katika hali ya fedheha.