Katika taarifa yake siku ya Jumanne, Wizara ya Mambo ya Nje ya Saudia imelaani matamshi ya matusi na ya kibaguzi yaliyotolewa na Waziri wa Fedha wa utawala wa Kizayuni dhidi ya taifa la Palestina.
Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Saudi Arabia imesema kuwa kuita matamshi yaliyo kinyume na ukweli kueneza matamshi ya chuki na vurugu kunadhoofisha misaada na juhudi za mazungumzo na amani ya kimataifa.
Katika taarifa yake hiyo, Wizara ya Mambo ya Nje ya Saudia iliunga mkono juhudi zote za kimataifa zinazolenga mapatano kati ya Palestina na utawala wa Kizayuni kwa kuzingatia mpango wa amani wa Waarabu na kudhamini kuundwa taifa la Palestina kwenye mipaka ya mwaka 1967 na mji mkuu wa Jerusalem Mashariki.
Msemaji wa Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Iran aidha amesema kuhusu matamshi ya kibaguzi ya Waziri wa Fedha wa Kizayuni Smotrich kwamba, matamshi ya kibaguzi na uchochezi ya Waziri wa Kizayuni dhidi ya haki mahususi ya Wapalestina katika ardhi ya kihistoria ya Palestina yanalaaniwa.
Amesisitiza kuwa, matamshi hayo yanadhihirisha wazi hali ya uchokozi na uchoyo wa utawala ghasibu wa Kizayuni dhidi ya mataifa yote ya eneo hili ikiwemo Jordan.
Waziri mwenye msimamo mkali wa fedha wa utawala wa Kizayuni ambaye hivi karibuni alizua utata kutokana na matamshi yake dhidi ya mji wa Hawara ulioko kusini mwa Nablus na ombi lake la kutaka kuharibiwa mji huu, ametoa kauli za ajabu wakati huu katika safari yake nchini Ufaransa. .
Bezalel Smotrich alidai kuwa hakuna taifa la Palestina na kwamba Wapalestina wamekuwepo kwa miaka 100!