Saudi Arabia kufanya mageuzi na mabadiliko katika bendera ya taifa, kufuta jina la Allah na la Mtume

Muhammad bin Salman mrithi wa kiti cha ufalme nchini Saudia ambaye kimsingi ndiye kiongozi wa nchi hiyo ameendelea kufanya mageuzi nchini humo ambapo sasa bendera na wimbo wa taifa kufanyiwa marekebisho.

Majlisi Shura ya Saudi Arabia ambayo ndio taasisi ya juu zaidi ya mashauriano ya utawala wa Kifalme imepasisha kwa wingi wa kura muswada wa kubadilisha wimbo wa taifa na bendera ya nchi hiyo.

Kwa mujibu wa mabadiliko hayo na kwa mujibu wa muswada huo uliopasishwa ni kuwa, mbali na wimbo wa taifa kufanyiwa mabadiliko jina tukufu la Mwenyezi Mungu na la Mtume (saw) “yaani Lailaha illallah, Muhammad Rasullah” yaliyoko katika bendera ya taifa ya nchi hiyo sasa yatafutwa. Bado haijabainika sababu hasa ya kuchukuliwa uamuzi huo.

Uamuzi huo tayari umeanza kukabiliwa na malalamiko na upinzani ndani ya Saudia huku Waislamu wa maeneo mengine wakijiuliwanmaswali yasiyo na majbu kuhusiana na uamuzi huo wa utawala wa Aal Saud.

Ikumbukwe kuwa, mwezi uliopita wa Januari, kuonyeshwa taswira za wanawake wanaodansi katika bararaba za mji wa Jazan nchini Saudi Arabia kulizusha taharuki na makelele mengi ya upinzani katika vyombo vya habari na mitandao ya kijamii pamoja na hasira na manung’uniko ya wananchi dhidi ya utendaji wa mrithi wa ufalme wa nchi hiyo.

Vyombo mbalimbali vya habari viliakisi wimbi la hasira za wananchi wa Saudia dhidi ya burudani zilizoanzishwa na Mohammad bin Salman, mrithi wa ufalme anayehisabika pia kama kiongozi halisi wa nchi hiyo, baada ya kuonekana wanawake wanaocheza dansi maarufu ya Brazil ya Samba wakiwa nusu utupu katika barabara za mji wa bandari wa Jazan kusini magharibi mwa nchi hiyo.

 

Previous Post
Next Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *