Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Saudi Arabia amesema kuwa, mazungumzo baina ya Iran na nchi yake yana matarajio mazuri na kwamba, nchi yake itaebndeleza mazungumzo na Tehran kwa jili ya kukutrubisha uhusiano.
Mnamo mwaka 2016, Saudi Arabia ilivunja uhusiano wake wa kidiplomasia na Iran kwa kisingizio cha kushambuliwa ubalozi wake mjini Tehran na ubalozi wake mdogo mjini Mash’had.
Mvutano wa Saudia na Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ulianza Januari 2016 baada ya Saudia kumnyonga mwanazuoni wa Kiislamu wa madhehebu ya Shia Sheikh Nimr Baqir al-Nimr. Kufuatia kunyongwa mwanazuoni huyo, waandamanaji wa Iran waliokuwa na hasira walivamia ubalozi wa Saudi mjini Tehran.
Hadi sasa kumefanyika duru tano za mazungumzo baina ya pande mbili katika mji mkuu wa Iraq Baghdad.
Faisal bin Farhan, Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Saudi Arabia amenukuliwa akisema kuuwa, Iran ni sehemu ya eneo na ni jirani yetu na sisi tutaebndeleza juhudi zenye lengo la kuhakikisha kunaweko ushirikiano baina yetu na Iran.
Iran daima imekuwa ikitangaza kuwa iko tayari kuendeleza mazungumzo na Saudi Arabia alimradi upande wa pili nao uonyeshe nia nzuri ya kushiriki kwenye mazungumzo ili yawe na matokeo yanayokusudiwa. Pamoja na hayo Saudia imekuwa ikishiriki kwenye mazungumzo hayo kwa tahadhari kubwa na inaonekana hilo linatokana na majivuno bandia iliyonayo ambayo yanaizuia kudhihirisha hadharani kuwa inayahitajia mazungumzo hayo ili kujiandalia fursa nzuri zaidi katika duru za baadaye za mazungumzo au huenda inaogopa kuukasirisha utawala haramu wa Israel.