Muungano vamizi Yemen unaoongozwa na Saudi Arabia umekiuka usitishaji vita mara 40 katika mkoa wa al Hudaidah.
Makundi ya Yemen yalisaini makubaliano ya kusitisha vita katika mkoa wa al Hudaidah kupitia mazungumzo ya Disemba 13 mwaka 2018 huko Stockholm Sweden, hata hivyo muungano vamizi wa Saudi Arabia na washirika wake tangu wakati huo umekiuka mara kadhaa makubaliano hayo na unaendelea kuwauwa raia wa Yemen.
Muungano vamizi wa Saudia umekiuka makubaliano ya kusitisha vita huko al Hudaidah ambapo hadi sasa umefanya mashambulizi ya makombora mara sita na kutekeleza mashambulizi mengine kwa kustafidi na silaha za aina mbalimbali.
Si hayo tu bali bali ndege za kijasusi za muungano vamizi wa Saudia zimeendelea kukiuka makubaliano hayo tajwa kwa kuruka katika anga ya eneo la His. Hii ni katika hali ambayo, Saudia pia inakiuka makubaliano ya kusitisha vita katika mikoa mingine ya Yemen ambapo muungano huo na mamluki wake katika kipindi cha saa 24 zilizopita umekiuka mara 131 makubaliano ya kibinadamu na kijeshi ya kusitisha vita huko Yemen.
Ali Qahum Mwakilishi wa Ofisi ya Kisiasa ya Harakati ya Ansarullah ya Yemen alishawatahadharisha wavamizi wa Saudia na kusisitiza kuwa, kamwe jeshi la Yemen halitakaa kimya mbele ya mashambulizi ya nchi hiyo na kwamba lina machaguo mengi mbele yake katika kujibu ukiukaji wa mapatano ya usitishaji vita unaofanywa na Saudi Arabia.