Serikali ya Jordan yaionya Israel kuhusiana na hujuma jinai zake dhidi ya Wapalestina

Wizara ya Mashauri ya Kigeni wa Jordan imeuonya utawala haramu wa Israel kuhusiana na kuendelea hujuma na mashambulio dhidi ya miji mbalimbali ya Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan, Palestina inayokaliwa kwa mabavu.

Taarifa ya Wizara ya Mashauri ya Kigeni wa Jordan iliyotolewa leo imetoa mwito wa kukomeshwa uvamizi unaofanywa na utawala ghasibu wa Isarel dhidi ya maeneo ya wananchi wa Palestina.

Aidha sehemu moja ya taarifa hiyo imesema bayana kwamba, hatua hizo za utawala ghasibuu wa Israel hazitakuwa na matokeo mengine ghairi ya kuongeza mizozo, mivutano na vitendo vya utumiaji mabavu huko Palestina inayokaliwa kwa mabavu.

Balozi Sinan al-Majal, msemaji rasmi wa Wiizara ya Mashauri ya Kigeni ya Jordan amesema kuwa, utumiaji mabavu unaofanywa na jeshhi la utawala haramu wa Israel hauna matokeo mengine ghairi ya kushadidisha vitendo vya ukandamizaji.

Jordan imeitaka pia jamii ya kimataifa kuliunga mkono taifa madhulumu la Palestina  ili lifanikiwe kufikia amani ya kiadilifu sambamba na kuhitimishwa uvamizi katika ardhi za wananchi madhulumu wa Palestina.

Katika miezi ya hivi karibuni vitendo vya hujuma na uvamizi wa walowezi wa Kizayuni katika maeneo ya Wapalestina hususan katika Msikiti wa al-Aqswa vimeongezeka mno.

Vitendo vya kuyavunjia heshima matukufu ya Kiislamu huko Palestina vinafanyika katika hali ambayo, viongozi wa nchi za Kiarabu na jamii ya kimataifa wameendelea kunyamaza kimya na kutochukua hatua zozote za maana za kukabiliana na vitendo hivyo vinavyokinzana na utu na ubinadamu.

Previous Post
Next Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *