Shambulio kubwa la udukuzi kwa utawala wa Kizayuni

Kufuatia shambulio la udukuzi dhidi ya utawala wa muda wa Kizayuni, kampuni kubwa zaidi ya usafiri ya utawala huo imeshindwa kuendelea na shughli zake.

Kwa mujibu wa Kundi la Kimataifa la Shirika la Habari la Fars, vyombo vya habari vya utawala wa muda wa Kizayuni viliripoti shambulio la mtandao lililoenea kwenye tovuti na seva za utawala huo.

Kuingana na ripoti ya Palestine Today, vyombo vya habari vya Kizayuni vilidai kuwa chanzo cha mashambulizi hayo ya mtandao ni nchi ya Iraq.

Kufuatia shambulio hilo, kampuni kubwa ya usafiri ya Igd katika Palestina inayokaliwa kwa mabavu ilifungwa na uwezekano wa kusajili shehena mpya kusitishwa.

Kwa mujibu wa ripoti hiyo, mfumo wa kituo kikuu cha usafiri wa umma kiichopo ndani ya Palestina iliyokaliwa kimabavu umevurugwa na kuzuia uwezekano wa kulipa kupitia kadi ya mkopo.

Aidha Huduma za reli ndani ya Palestina inayokaliwa kimabavu zilisitishwa kufuatia shambulio hilo la mtandao.

Hii sio mara ya kwanza kwa tovuti na seva za Kizayuni kulengwa na mashambulio ya mtandao kutoka Iraq.

Hapo awali wadukuzi hao wameshambulia tovuti na seva za Uwanja wa Ndege wa Bangorion mjini Tel Aviv na vituo vingine kadhaa.

Previous Post
Next Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *