Sheikh Ikrima Sabri: Quds na Msikiti wa al-Aqswa vinapitia kipindi kigumu

Khatibu wa msikiti mtakatifu wa al-Aqswa huko Palestina amesema kuwa, Quds na Msikiti wa al-Aqswa vinapitia kipindi kigumu kabisa.

Sheikh Ikrima Sabri amesema kuwa, moto katika Msikiti mtakatifu wa al-Aqswa ambao ni kibla cha kwanza cha Waislamu bado haujazimika.

Akizungumza kwa mnasaba wa kumbukumbu ya mwaka ambao Wazayuni walikichoma moto Kibla cha Kwanza cha Waislamu yaani Msikiti wa al Aqsa huko Palestina.

Khatibu wa msikiti wa al-Aqswa ameeleza kuwa, moto dhidi ya msikiti huo ungali unawka kupitia vitendo kama vya kuuvamia msikiti huo mara kwa mara uvamizi ambao unafanywa na walowezi wa vingoji vya Kizayuni.

Kadhalika amesema, kuporwa ardhi za Wapalestina, kuyayahudisha maeneo ya Wapalestina, kamatakamata ya kiholela na kuwalazimisha Wapalestina kuwa wakimbizi na hatua mbalimbali za kibaguzi zinazofanywa na viongozi wa utawala ghasibu yote hayo ni mifano ya wazi kabisa inayoonyesha kuwa, moto dhidi ya msikiti wa al-Aqswa ungali unawaka na hauujazimika.

Tarehe 21 Agosti 1969 Mzayuni mmoja aliuchoma moto Msikiti huo ukiwa ni uthibitisho mwingine wa jinai kubwa za utawala wa Kizayuni.

Tukio hilo la kuuchomwa moto Msikiti wa al-Aqswa liliamsha hasira na ghadhabu za Waislamu duniani kote. Aidha utawala wa Kizayuni uliilinasibisha tukio hilo na mtalii mmoja Myahudi mwenye misimamo ya kufurutu ada raia wa Australia aliyejulikana kwa jina la Denis Michael. Mtalii huyo alifikishwa mahakamani na kuhukumiwa kimaonyesho tu na kisha akaachiwa huru kwa madai kwamba eti alikuwa mgonjwa wa akili.

Previous Post
Next Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *