Sheikh Issa Qassim: Kujengwa kitongoji cha walowezi wa Kiyahudi Manama ni jinai

Kiongozi wa Harakati ya Kiislamu ya Bahrain amekosoa viikali uamuzi wa utawala wa Aal Khalifa wa kuanzisha kitongoji cha walowezi wa Kiyahudi katika mji mkuu Manama na kueleza kwamba, hatua hiyo ni jinai na dhulma ya wazi dhidi ya wananchi wa nchi hiyo ya Kiarabu.

Sheikh Issa Qassim, kiongozi wa kimaanawi wa Mapinduzi ya Wananchi wa Bahrain amesisitiza katika taarifa yake kwamba, kujenga kitongoji cha walowezi wa Kiyahudi katika mji wa Manama maana yake ni kubadilisha utambulisho wa kitaifa, Kiislamu na Kiarabu  na vile vile kitendo hicho kinapotosha historia ya nchi pamoja na nyaraka zake.

Ayatullah Issa Qassim ameongeza kuwa, kitendo hicho cha viongozi wa Manama kitawafungulia milango wavamizi wa Kizayuni na hivyo kupanga njama kwa urahisi na utawala wa Aal Khalifa.

Kiongozi wa Harakati ya Kiislamu ya Bahrain sambamba na kupinga vikali uamuzi huo ameeleza bayana kwamba, kufanya hivyo ni kutenda dhulma ya wazi dhidi ya wananchi wa nchi hiyo pamoja na historia ya nchi yao.

Radiamali hiyo ya Sheikh Issa Qassim inafuatia kutangazwa mpango wa utawala wa Aal Khalifa wa kubadilisha kwa takribani asilimia 40 ya vitongoji vya kale katika mji wa Manama na kuvipa nembo na utambulisho wa Kiyahudi.

Tayari hivi sasa kuna ununuzi usiokoma wa majengo hayo ya kale tena kwa bei ya juu lengo likiwa ni kulibadilisha eneo hilo baadaye na kulifanya kuwa kitongoji cha walowezi wa Kiyahudi.

Previous Post
Next Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *