Sheikh Kazem Seddiqi: Marekani imeshindwa kuupatia ufumbuzi mgogoro wa ndani wa Israel

Khatibu wa Swala ya Ijumaa iliyoswaliwa leo hapa mjini Tehran amesema kuwa, licha ya Marekani kuwa na mfungamano wote na utawala haramu wa Israel lakini imeshindwa kuupatia ufumbuzi mgogoro wa ndani wa utawala huo, na hilo ni ishara ya kutokuwa na uwezo.

Hujjatul Islam wal Muslimin Sheikh Kazem Seddiqi amesema hayo leo mbele ya hadhara kubwa ya waumini waliohudhuria ibada ya kimaanawi na kisiasa ya Swala ya Ijumaa hapa Tehran ambapo sambamba na kubainisha kwamba, pembe kali ya Marekani katika sera za kigeni walikuwa Wazayuni ameeleza kuwa, hivi sasa Israel inashuhudia maandamano ya mamia ya maelfu ya watu na hivyo kupitia katika kipindi kigumu cha mgogoro mkubwa zaidi katikak historia yake.

Khatibu wa Swala ya Ijumaa mjini Tehran amesema pia kuwa, uwezo na nguvu ya kambi ya muqwawama iko kwa namna ambayo eneo la Ukingo wa magharibi wa Mto Joradn limejizatiti kwa silaha na kila siku kunatekelezwa operesheni ya kijeshi dhidi ya Wazayuni, kiasi kwamba, hata shakhsia wakubwa wa Kizayuni wamejitokeza na kusema kuwa, utawala huo hautafikisha miaka 80 katika umri wake.

Aidha amesema, satua ya Marekani nje ya mipaka yake kila siku inazidi kuporomoka na nguvu yake inadhoofika, ambapo kipindi fulani eneo la Amerika ya Latini lilikuwa sehemu ya kujifaragua Marekani, lakini hii leo wanachaguliwa Marais ambao misimamo yao iko dhidi ya ubeberu wa dunia.

Kuhusiana na vikwazo vya Marekani, Sheikh Kazem Seddiqi amesema kuuwa, vikwazo vya Marekani dhidi ya Iran havijaweza kufikia malengo yaliyoainishwa, kwani Washington ilikuwa ikidhani kwamba, ingeweza kuyapigisha magoti Mapinduzi ya Kiislamuu ya Iran.

Previous Post
Next Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *