Sheikh Naim Qassem: Hizbullah itatoa jibu kali kwa Saudi Arabia

Naibu Katibu Mkuu wa harakati ya Hizbullah ya Lebanon amelaani matamshi yaliyotolewa hivi karibuni na mfalme wa Saudi Arabia kuhusu harakati hiyo na kusema kuwa, hatua hiyo inachochea machafuko nchini Lebanon na kwamba Hizbullah itatoa jibu kali kwa uchochezi huo.

Sheikh Naim Qassem ambaye alikuwa akizungumza kwa mnasaba wa kukumbuka mwaka wa pili wa kuuawa shahidi Kamanda Qasem Soleimani katika hafla iliyofanyika kwenye mji wa Nabatieh amesema kuwa, matamshi yaliyotolewa na Mfalme wa Saudia akiitaja harakati ya Hizbullah kuwa ni kundi la kigaidi ni tuhuma dhidi ya sehemu kubwa ya jamii ya Lebanon na vikosi vya muqawama na wanamapambano ambao wana taathira kubwa katika eneo la Magharibi mwa Asia.

Sheikh Naim Qassem, haikubali kabisa hatua hiyo ya Saudi Arabia ya kuivunjia heshima harakati hiyo na itatoa jibu madhubuti na la kimantiki kwa utawala huo. Akiinyooshea kidole Saudi Arabia, Sheikh Naim Qassem amesema: Gaidi ni utawala unaokandamiza itikati tofauti ndani ya nchi yake mwenyewe, kuwashambulia majirani zake na kuhalalisha hatua zote za kuanzisha uhusiano na utawala haramu wa Israel kwa njia mbalimbali.

Katika hotuba yake ya mwaka aliyoitoa hivi karibuni mfalme wa Saudi Arabia aliitaja Hizbullah ya Lebanon kuwa ni kundi la kigaidi na kuwataka watu wa Saudia kukabiliana na harakati hiyo.

Previous Post
Next Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *