Sheikh Naim Qassem: Israel haina budi kutambua rasmi haki za maliasili za Lebanon

Naibu Katibu MKuu wa Hizbullah ya Lebanon amesema, utawala haramu wa Kizayuni wa Israel hauna budi kuzitambua rasmi haki za Lebanon zinazohusiana na utajiri wa maliasili za baharini.

Sheikh Naim Qassem ameyasema hayo katika majlisi kuu ya Ashura na kusisitiza kuwa, Wamarekani inawapasa waache kushirikiana na Wazayuni katika kutafuta na kuchimba gesi katika eneo la Lebanon.

Sheikh Naim Qassem ameongezea kwa kusema: “Sisi tumeweza kuushinda utawala wa Kizayuni na kulitokomeza genge la DAESH kwa kufuata njia ya Imam Hussein (AS)”.

Naibu Katibu Mkuu wa Hizbullah amebainisha pia kwa kusema: “ikiwa baadhi ya watu wanarudi nyuma katika suala la kukomboa ardhi zetu, sis hatutarudi nyuma katika hilo. Kama tutakuwa na uwezo wa kuifanya kazi hiyo na wengine wakawa hawana uwezo wa kufanya hivyo, tutawapa msaada kulifanikisha hilo”.

Katika sehemu nyingine ya hotuba yake, Naibu Katibu Mkuu wa Hizbullah amesema, Marekani imefikia kilele cha kufanya ufisadi duniani; na wakati mtu anapoikimbilia Washington ili kupata hifadhi, ni wazi kuwa ataishia kufuata njia ya hila, urongo, uzandiki na upotofu.

Halikadhalika, mbali na kutoa indhari kwamba endapo adui atatoa vitisho dhidi ya Lebanon muqawama utachukua hatua kukabiliana na vitisho hivyo, Sheikh Naim Qassem amesisitiza kuwa, katika kukamilisha nafasi ya muqawama, Hizbullah itashirikiana na serikali ya Lebanon ili kuifanya iwe imara na yenye nguvu katika kupigania haki zake.

Hatua iliyochukuliwa na utawala wa Kizayuni wa Israel yapata miezi miwili nyuma, ya kutuma meli ya ugunduzi wa gesi ya Energean katika eneo la mpaka wa majini la Karish linalozozaniwa na Lebanon na utawala huo, imeibua mvutano mpya  baina ya Beirut na Tel Aviv na kulifikisha kileleni suala la kupigania haki za mafuta na gesi ya Lebanon katika Bahari ya Mediterania.

Previous Post
Next Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *