Naibu Katibu Mkuu wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Kiislamu ya Hizbullah ya Lebanon amesema kuwa, Marekani daima imekuwa ikifutilia kuzusha vurugu na machafuko nchinii Lebanon.
Samahat Sheikh Sheikh Naim Qassim, Naibu Katibu Mkuu wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Kiislamu ya Hizbullah ya Lebanon ameeleza kuwa, hii leo Marekani inaunga mkono utawala ghasibu wa Israel na mipango michafu ya kuibomoa Lebanon.
Kiongozi huyo wa ngazi za juu wa Chama cha Hizbullah amebainisha kuwa, kuna sababu nyingi zinazoifanya Lebanon iweko katika hali ya kusambaratika kama ufisadi na uongozi mbaya lakini sababu kuu ni vikwazo vya Marekani ambapo Washington daima imekuwa ikifanya njama za kuzusha vurugu na machafuko katika nchi hiyo.
Aidha Sheikh Naim Qassim ameutawala utawala wa kibaguzi wa Israel kama tishio halisi na kutoa mwito wa kuwa macho na nyendo za utawala huo vamizi unaotenda jinai kila uchao dhidi ya wananchi wa Palestina.
Ripoti mbalimbali zinaonyesha kuwa, muqawama hivi sasa ni imara na una nguvu zaidi kuliko wakati mwingine wowote na kwa taufiki ya Allah na jitihada kubwa na baraka za damu za mashahidi, leo hii tunaiona Lebanon ikiwa nchi yenye nguvu na inayoamua mambo yake na kuyatekeleza bila ya woga.
Mafanikio iliyopata hivi karibuni Lebanon ya kuulazimisha utawala wa Kizayuni ufanye haraka kushiriki katika uchoraji wa mipaka ya baharini na kukubali masharti ya Beirut, kwa hakika ni ushindi mkubwa kwa taifa la Lebanon.