Kiongozi wa Harakati ya Kiislamu ya Nigeria alitangaza kuwa, operesheni ya adhabu ya Iran dhidi ya utawala wa Kizayuni ilifufua matumaini katika nyoyo za watu wanaodhulumiwa na kukandamizwa duniani.
Sheikh Ebrahim Zakzaky, Kiongozi wa Harakati ya Kiislamu ya Nigeria akiashiria operesheni ya adhabu ya Iran ya “Ahadi ya Kweli” dhidi ya utawala wa Kizayuni ametangaza kuwa, mashambulizi ya Iran dhidi ya Israel yalizua matumaini katika nyoyo za madhulumu na wanaodhulumiwa duniani. wa imani.”
Alitoa kauli hizi katika mkutano na maafisa wa taasisi za kidini na wanaharakati wa kijamii nchini Nigeria.
Huku akisisitiza kuwa, mashambulizi ya IRGC dhidi ya Israel yatauzuia utawala huo kufanya jinai zaidi, ameongeza kuwa: Ujumbe wa shambulizi hili ulikuwa kwamba, iwapo utawala huo ungetutishia hadi hivi sasa, basi ni wakati wa wao kuonja tishio letu.
Sheikh Zakzali ameongeza kuwa: Dhana ya kutoshindwa Israel iliyokuwa imeenea katika fikra za baadhi ya watu, ilisambaratishwa na hujuma ya Iran dhidi ya utawala huo na ikaonyesha kwamba kile kilichofikiriwa ni ndoto na dhana tu.
Kiongozi wa Harakati ya Kiislamu nchini Nigeria pia alisema: Nilishangaa sana niliposikia mtu akilia kwa furaha, lakini niliposikia kwamba Iran ililipiza kisasi dhidi ya shambulio la Israel dhidi ya ubalozi wake mdogo nchini Syria, nilifurahi sana na kutoa machozi ya furaha.