Shetani kudhihiri katika mfano wake halisi Katika sinema za Hollywood

Kituo cha Utafiti wa Mambo ya Kizayuni cha Faraan: Kuna vikundi kadhaa vya filamu zilizotengenezwa Hollywood kuhusiana na shetani: Katika baadhi ya sinema, kama vile ‘Harry Potter’ na ‘Lord of the Rings’, zinaashiria ya kwamba shetani ni mwenye nguvu nyingi; Ingawa ndani yake hamna utajo wa Mungu. Katika baadhi ya simema zenginezo, kama vile ‘Ghostbusters’ na ‘Astrology’ ya kwanza, ya pili na ya tatu zinamtaja Yesu Kristo na pia vilevile kwa kando yake zinamtaja Shetani. Lakini ukuzaji wa woga kutokana na nguvu za shetani ni jambo ambalo kwamba linatangazwa kupitia kazi (sinema) hizi. Baadhi ya kazi hizi zinaonyesha Shetani akiwa kando ya Mungu. Katika sinema zengine huleta katika taswira zikionyesha kua shetani anamiliki nguvu zaidi ya Mungu. Kama vile sinema za kutisha ya Constantine nambari ya 4 na ya 5.

Kumuogopa shetani na uwezo wake ni utangulizi wa kujisalimisha kwake na hupelekea kukata tamaa kutokana na rehema ya Mungu na hatimaye kuelekea kwake shetani na kumuabudu. Yeyote anayemuogopa shetani au kiumbe chochote kile kwa hakika anakua amejisalimisha kwake na uwezo wake na hatimaye unakua mtumwa wake. “Qurani Tukufu” inasema: ‘Hakika huyo ni Shet’ani anawatia khofu marafiki zake, basi msiwaogope, bali niogopeni Mimi mkiwa nyinyi ni Waumini’.

Katika filamu nyingi zenye mada ya kidini, aina ya wovu wa Ibilisi au mfano halisi wa shetani shetani ni jambo la wazi.

Mara nyingi mfumo wenye kutisha na wenye kuleta hamasa hutumika katika filamu hizo zilizo na maudhui ya shetani, kama vile matumizi ya rangi nyeusi, rangi nyekundu, rangi ya njano, na wakati mwingine anga ya bluu katika sehemu zenye ishara ya uovu, ikiambatana na vumbi na mapigo ya radi, ni mambo yenye nafasi maalum.
Wanyama kama vile nge, nyoka, au joka lenye mabawa na lenye pembe, popo, mbwa mweusi, buibui, mbweha, kunguru, mbuzi na nyati (viumbe wenye rangi nyekundu, ishara ya moto wa kuzimu, mkia na mkuki mkononi) ni katika alama za Shetani na wafuasi wake.

Ishara nyengine kama vile msalaba uliogeuzwa, mpevu uliogeuzwa, koni ya obeliski, nyota yenye ncha tano na sita katika duara yenye herufi za Kiebrania au peke yake, nyuso zenye muonekano mbaya, fuvu la kichwa na mfupa, mifupa isiyo na nyama, upanga wa damu, pembetatu na duara zisizolingana kando kando, Miduara isiyo kamili na kituo kimoja, ni katika alama muhimu zaidi za ushetani ambazo zenyewe zinachukua sehemu ya shetani.

Nambari kama vile 666, 3, 6, na 13 huwa ni nambari zenye muonekano wa kutisha katika baadhi ya sinema.

Vurugu, umwagaji damu, uchawi, unabii, vitisho, kukata tamaa, giza na weusi ni sifa kuu za simulizi za shetani zinazoonyesha nguvu za shetani na vilevile kwa kupitia muziki mbaya katika kuita roho ya hadhira kujisalimisha na kunyenyekea kwa shetani na zaidi kuchochea hisia.Kama ambavyo jeuri na ushenzi, huvuruga usawa wa kiakili wa hadhira na kumnyima muathiriwa uwezo wa kufikiri hadi mwishowe kumuathiri.

Chanzo: Mohammad Hossein Farajnejad, hadithi za Kizayuni za sinema

Previous Post
Next Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *