Shirika la Afya Dunia (WHO): Mpox sio “Covid” mpya

Shirika la Afya Dunia (WHO) limesema kuwa ugonjwa wa Mpox, pamoja na aina zake mpya na za zamani, sio janga jipya kama “Covid,” kwani maafisa husika wanajua jinsi ya kudhibiti kuenea kwake.

Mkurugenzi wa shirika hilo barani Ulaya, Hans Kluge, alieleza – jana katika mkutano na waandishi wa habari – kwamba “Mpox sio Covid mpya; iwe ni aina ya 1 inayosababisha janga la sasa katika Afrika ya Kati na Mashariki, au aina 2 ya Mpox ambayo ilikuwa sababu ya kuzuka janga hilo duniani mnamo 2022.”

Kluge amesisitiza haja ya kupambana na janga na Mpox kote duniani.

Shirika la Afya Duniani limeutangaza mlipuko wa hivi sasa wa Mpox kuwa ni dharura ya afya ya umma ambayo inatia wasiwasi kimataifa baada ya kugunduliwa kwa aina hiyo mpya.

Barani Afrika, mlipuko wa ugonjwa wa Mpox umeripotiwa katika nchi za Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Burundi, Kenya, Rwanda na Uganda.

Mawaziri wa Afya wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC) wanatarajiwa kukutana hivi karibuni kwa ajili ya kujadili virusi vya homa ya Mpox ambavyo vinaenea kwa kasi  katika maeneo tofauti ya dunia.

Previous Post
Next Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *