Waziri Mkuu wa Serikali ya Mamlaka ya Ndani ya Palestina amesema, serikali mpya ya utawala haramu wa Kizayuni wa Israel chini ya uongozi wa wanasiasa wa mrengo wa kulia wenye misimamo ya kufurutu ada inajiandaa kutangaza vita dhidi ya Wapalestina.
Kwa mujibu wa shirika la habari la Palestina SAMA, Muhammad Ashtiyeh, amebainisha kuwa mazungumzo ya uundaji baraza la mawaziri la Israel yanafanyika kwa msingi wa kuhakikisha ni nani ataweza kujenga vitongoji zaidi vya walowezi wa Kizayuni na nani anayetaka kurahisisha kazi ya kuwafyatulia risasi Wapalestina na kutaifisha ardhi nyingi zaidi za Wapalestina.
Tarehe 13 Novemba, rais wa utawala wa Kizayuni Yitzhak Herzog alimkabidhi rasmi Benjamin Netanyahu, kiongozi wa muungano wa mrengo wa kulia wenye misimamo ya kufurutu mpaka jukumu la kuunda baraza jipya la mawaziri.