Wawakilishi wa ngazi ya juu wa makundi ya mapambano, vyama vya kisiasa vya Lebanon na harakati za mapambano ya ukombozi za Palestina zimeshukuru na kupongeza misaada na uungaji mkono wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.
Makundi hayo yametoa pongeza na shukrani hizo katika hafla ya kumalizika muda wa kuhudumu balozi wa Iran mjini Beirut.
Muhammad Jalal Firouznia aliyekuwa balozi wa Iran mjini Beirut Lebanon tangu tarehe 30 Juni mwaka 2018, amemaliza muda wake katika nafasi hiyo.
Katika hafla hiyo iliyofanyika Beirut, wawakilishi wa ngazi ya juu wa makundi ya muqawama wa Kiislamu, vyama vya kisiasa vya Lebanon na Palestina wamepongeza uungaji mkono na misaada ya Iran kwka harakati za kupigania haki na uadilifu na kusema: Jamhuri ya Kiislamu iko mstari wa mbele katika kukabiliana ubeberu na maadui wa wanaadamu wa mataifa ya kanda hii.
Muhammad Jalal Firouznia pia amesema katika hafla hiyo kuwa, Jamhuri ya Kiislamu ya Iran siku zote imekuwa pamoja na marafiki zake na katika safu ya kwanza ya muqawama. Amesema, muqawama na mapambano ni kigezo muhimu zaidi cha kuyakurubisha pamoja mataifa ya eneo la Magharibi mwa Asia.