Gazeti la Israel la Ma’ariv lilichapisha mahojiano yake na mwanasiasa wa Israel kuhusu mpango wa siri wa Benjamin Netanyahu wa kusalia madarakani kwa kuahirisha uchaguzi wa 2026.
Katika tovuti yake, Gazeti hili lilichapisha mahojiano yake pamoja na mwanasiasa wa Israel mwenye mafungamano na chama cha Likud ambaye hapo awali alifanya kazi na waziri mkuu anayekalia kwa mabavu (Benjamin Netanyahu), ambapo alizungumzia matamanio yake na kiu chake kisichoisha cha kutaka kuendelea kukaa madarakani hata ikiwa italazimu kuvuruga uchaguzi wa mwaka 2026.
Mwanasiasa huyo wa Israel alifichua kuwa Netanyahu anategemea Rais wa Marekani Donald Trump ili kupata mamlaka katika uchaguzi ujao wa rais wa Marekani ili kuhakikisha kuendelea kwa utawala wake.
Kwa mujibu wa gazeti hili, mwanasiasa huyu mkongwe kutoka chama cha Likud, ambaye alifanya kazi kwa karibu na Netanyahu kama mshauri, alisisitiza: “Netanyahu atasalia kuwa waziri mkuu kwa angalau miaka 5.”
Mwanachama wa Likud alielezea: “Kinachotokea sasa katika idara ya polisi ni mwanzo tu. Hivi karibuni, wakuu wote wa huduma za usalama, iwe jeshi la Israeli, Mossad au Shin Bet, watamaliza majukumu yao. “Netanyahu huteua mtu ambaye ni mwaminifu kwake pekee katika hali yoyote.”
Mwanasiasa huyu alidokeza kwamba Netanyahu ana malengo mawili: kwanza, kusukuma mzozo wa kaskazini (mpaka wa pamoja wa Palestina inayokaliwa kwa mabavu na upande wa kusini mwa Lebanon) hadi kufikia hatua ya mlipuko, pili, kugombana na Biden na kumtumikia Trump.
Kulingana naye, baada ya kuingia madarakani, Trump atampa Netanyahu uhuru wa kuanzisha vita kamili na vya muda mrefu na Lebanon, ambayo itazuia kufanyika kwa uchaguzi.
Haya yote pamoja na kukamilika kwa mchakato wa kukamata mifumo ya ndani kunamruhusu Netanyahu kuahirisha uchaguzi na kusalia madarakani.