Sisitizo la kulaaniwa kuvunjiwa heshima Msikiti wa Al-Aqsa

Nchi za Kiarabu na Kiislamu zimesisitiza ulazima wa kulaaniwa kitendo cha Waziri wa Usalama wa Ndani wa utawala ghasibu wa Israel cha kuuvunjia heshima Msikiti wa Al-Aqsa.

Itamar Ben-Gvir, Waziri mpya wa Usalama wa Ndani wa utawala wa Kizayuni, Jumanne asubuhi, na ikiwa ni katika wiki yake ya kwanza ya kazi akiwa na kundi jingine la Wazayuni waliokuwa wanasindikizwa na jeshi la utawala huo ghasibu, walifanya uchochezi mkubwa na kuuvunjia heshima Msikiti wa Al-Aqsa kwa kuingia msikitini humo bila kujali lolote.

Kuhusiana na hilo, nchi za Kiarabu na Kiislamu zimelitaka Baraza la Usalama, kuandaa kikao leo Alhamisi kwa ajili ya kujadili suala la Palestina na kulaani hadharani kitendo cha Itamar Ben Gvir, Waziri wa Usalama wa Ndani wa utawala ghasibu wa Israel cha kuingia katika msikiti huo mtakatifu.

Riyad Mansour, Mwakilishi wa Mamlaka ya Ndani ya Palestina katika Umoja wa Mataifa amewaambia waandishi wa habari kwamba jamii ya kimataifa ina jukumu la kuhifadhi hali ya kihistoria ya Beitul Muqaddas na kutetea maeneo yake ya Kikristo na Kiislamu.

Mansour amesisitiza kwamba Waislamu wanataka uvunjiwaji heshima Msikiti wa Al-Aqsa usirudiwe tena na kuhakikisha kwamba maeneo matakatifu ya Al-Quds yanaheshimiwa kweli na si kwa maneno matupu tu.

Mwakilishi wa Mamlaka ya Ndani ya Palestina katika Umoja wa Mataifa amesema: Wote wameungana dhidi ya hatua hii ya itikadi kali ya utawala wa Israel na wahusika wake kama vile Itamar Ben Gvir, waziri aliyevamia na kuuvunjia heshima Msikiti wa Al-Aqsa.

Msikiti wa Al-Aqsa unajulikana kuwa nembo kuu ya utambulisho muhimu wa Kiislamu na Palestina mjini Beitul Muqaddas na utawala wa Israel unajaribu kuharibu umuhimu huo, lakini kusimama na kuwa macho wananchi wa Palestina kumeufedhehesha utawala wa Kizayuni na kuufanya ushindwe kufikia malengo yake maovu dhidi ya Waarabu na Waislamu.

Previous Post
Next Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *