Baraza la Wanachuo wa Shule ya Sheria ya Chuo Kikuu cha New York nchini Marekani limetangaza rasmi kuiunga mkono Harakati ya Vikwazo na Kuususia Utawala ghasibu wa Israel (BDS).
Faraan: Wanachama wa Baraza hilo la Chuo Kikuu cha New York Marekani wamepiga kura zao zote na kuituhumu Israel kuwa inazikalia kwa mabavu na kuzikoloni ardhi za Palestina na kutenda jinai na ukandamizaji dhidi ya Wapalestina kwa kuwapatia maafisa wa ngazi ya juu wa kijeshi zana za kijeshi, silaha, ndege zisizo na rubani, teknolojia ya kijeshi, mafunzo na nyadhifa.
Baraza hilo pia limeituhumu taasisi za elimu za Israel kuwa zinahusika moja kwa moja katika ubaguzi wa rangi, mauaji ya halaiki na jinai za kivita. Baraza la Wanachuo wa Shule ya Sheria ya Chuo Kikuu cha New York nchini Marekani limetaka kusitishwa mpango wa kubadilishana wanachuo na utawala wa Kizayuni na kujiunga na harakati ya BDS.
Wakati huo huo wanachuo wa Skuli ya Sheria katika Chuo Kikuu cha New York wamesema kuwa mabadilishano ya kitaaluma baina yao na vyuo vikuu vya Israel ni aina fulani ya propaganda inayofanyika kuunga mkono sera za kikoloni na kibaguzi za maghasibu wa Kizayuni.
Baraza la Wanachuo wa Skuli ya Sheria ya Chuo Kikuu cha New York Marekani linaamini kuwa taasisi za kielimu za Israel zinawabagua wanachuo wa Kipalestina na kuzima sauti ya kuunga mkono mapambano ya ukombozi wa Palestina kwa ajili ya kupigania haki yao ya kujiainishia mustakbali wao.