Syria: Tutatumia haki yetu ya kisheria kujibu jinai za utawala haramu wa Israel

Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Syria imetangaza kuwa, mashambulio ya utawala ghasibu wa Israel dhidi ya Uwanja wa Ndege wa Halab ni jinai za kivita na kwamba, Damascus itatumia haki yake ya kisheria kwa ajili ya kujibu jinai za utawala huo.

Taarifa iliyotolewa na Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Syria imeeleza kwamba, mashambulio ya mara kwa mara ya utawala haramu wa Israel hususan hatua yake ya kulenga kwa makusudi maeneo ya raia likiwemo shambulio la hivi karibuni dhidi ya Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Halab kwa mujibu wa sheria za kimataifa yanahesabiwa kuwa ni jinai za kivita.

Sehemu nyingine ya taarifa hiyo imebainisha kwamba, kwa kufanya mashambulio hayo, kwa mara nyingine tena viongozi wa Israel wamehatarisha amani na usalama wa eneo sambamba na roho na uhai wa raia.

“Syria itatumia kila wenzo na suhula na kwa nguvu zake zote kwa ajili ya kutetea ardhi zake ambayo kimsingi ni haki yake ya kisheria, imesisitiza taarifa hiyo.

Jumatano ya jana jeshi la utawala ghasibu wa Israel lilishambulia kwa makombora kadhaa viwanja vya ndege wa Kimataifa vya Halab na Damascus.

Mashambulizi ya kijinai ya utawala wa Kizayuni wa Israel na Marekani nchini Syria yamekuwepo tangu miaka kadhaa nyuma tangu ulipoundwa muungano eti wa kimataifa wa kukabiliana na magaidi wa Daesh.

Mashambulio hayo yanafanyika katika hali ambayo, Syria imetuma barua mara kadhaa katika Umoja wa Mataifa kulaani na kutaka kusitishwa mashambulio hayo, ingawa hadi sasa Umoja wa Mataifa haujachukua hatua yoyote ya maana katika uwanja huuo.

Previous Post
Next Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *