Tabia inayofanana na ISIS ya wanajeshi wa Israeli katika kuwakamata raia wa kipalestina mjini Gaza

Kusambaa kwa picha za kukamatwa kwa umati  wa raia wakipalestina mjini Ghaza na jeshi la utawala wa Kizayuni kumesababisha taathira kubwa katika mitandao ya kijamii na maoni ya wananchi kote duniani.

Askari wa utawala wa Kizayuni wamsambaza picha za kukamatwa kwa umati wa watu wa Ghaza waliolala chini huku mikono yao  na macho yao yakiwa yamefungwa, kumezusha hisia nyingi miongoni mwa maoni ya wananchi ulimwenguni.

Baadhi ya watumiaji wa mitandao ya kijamii wamelinganisha tabia ya Wazayuni na tabia ya magaidi kwa kuchapisha picha za tabia ya ISIS wakiwa na wafungwa wake huko Syria na Iraq na kuzilinganisha picha hizi mbili pamoja.

Haya yalijiri wakatih ushahidi ukionyesha kuwa watu waliokamatwa na jeshi la Kizayuni hawana uhusiano wowote na vikosi vya kundi la muqawama au Hamas na wote ni miongoni mwa watu wa kawaida katika mji wa Ghaza.

Hadi al-Mazoon, ambaye ni mkuu wa masuala ya kibinadamu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi wa Kipalestina linalojulikana kama UNRWA, alisema katika mahojiano na CNN: “Ninawafahamu watu wengi waliopo kwenye picha hii.”

Katika mahojiano na ripota wa CNN, aliongeza: “Sio wafungwa wala si wapiganaji wa Hamas; “Ni raia tu ambao walikuwa huko na familia zao na walijaribu kuitoroka hali hii.”

Al-Mazoon anaendelea: Nimechanganyikiwa na kushtuka kuona baba yangu, kaka yangu na muuza duka wakitolewa nje ya nyumba yao na kukamatwa kama wapiganaji wa Hamas.

Aliongeza zaidi: Walimvua nguo ndugu yangu ambaye ana kifafa na kumweka ufukweni kwenye baridi.

Mfanyikazi huyu wa shirika la Umoja wa Mataifa aliongeza: Familia yangu ilikaa kaskazini mwa Gaza kwa sababu hawakuwa na mahali pa kwenda kusini. Mwisho haijalishi tupo wapi kuna uwezekano wa kuuawa kwanini tuhangaike twende kusini.

Mtandao Mpya wa Kiarabu uliripoti kuhusu picha hii; Mwandishi wa habari maarufu wa Kipalestina aitwaye Zia Kalhut, anayefanya kazi na Mtandao Mpya wa Kiarabu, ametambuliwa miongoni mwa waliokamatwa. Mtandao huu ulitangaza kuwa mwandishi wake alikamatwa pamoja na ndugu na jamaa zake pamoja na raia wengine.

Hii sio mara ya kwanza kwa Wazayuni kuwatendea Wapalestina hivi. Kwa mujibu wa takwimu za Umoja wa Mataifa, takriban asilimia 98 ya Wapalestina katika jela za Israel, baadhi yao walibadilishana hivi majuzi wakati wa usitishaji vita, hawana mashtaka yoyote na walifungwa jela bila kufuata utaratibu.

Al Jazeera pia imeripoti kuwa, hivi karibuni wanajeshi wa Kizayuni walimtumia mfungwa wa Kipalestina kama ngao ya binadamu wakati wa shambulio dhidi ya kambi ya wakimbizi wa Kiarabu katika Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan.

Ezzat al-Rashq, mjumbe wa ofisi ya kisiasa ya Hamas, aliishutumu Israel kwa utekaji nyara, kutafuta kwa nguvu na kuwanyang’anya kundi la wakimbizi wa Kipalestina katika taarifa.

Watu wengi wa kaskazini mwa Gaza walikataa kuhamia eneo la kusini licha ya onyo la utawala wa Kizayuni kuwalazimisha kuhamia kusini mwa Gaza. Kwa upande mwingine, wakati wa usitishaji vita wa wiki moja, wakimbizi wengi wa Kipalestina waliokuwa wamekwenda kusini walirejea makwao.

Wachunguzi wa masuala ya kisiasa wanasema kuwa, utawala wa Kizayuni ambao umekata tamaa katika kukabiliana na muqawama wa Hamas na haujapata maendeleo makubwa katika vita na vikosi vya Hamas na uharibifu wa mahandaki yake, unalipiza kisasi kwa wananchi na raia wa Ghaza.

Previous Post
Next Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *