#afghanistan

Mashirika makubwa ya misaada yasitisha shughuli Afghanistan baada ya Taliban kupiga marufuku wafanyakazi wa kike

Mashirika makubwa ya misaada yasitisha shughuli Afghanistan baada ya Taliban kupiga marufuku wafanyakazi wa kike

Mashirika kadhaa yasiyo ya kiserikali (NGOs) yamesitisha shughuli zake nchini Afghanistan baada ya serikali ya Taliban kupiga marufuku wanawake kufanya kazi katika mashirika hayo. Ripoti kutoka nchini humo zinasema kuwa, mashirika kadhaa makubwa ya kigeni yasiyo ya kiserikali nchini Afghanistan jana yalisimamisha shughuli za kibinadamu ikiwa ni, siku moja tu baada ya Taliban kuwazuia kuajiri…

Al-Azhar: Hatua ya Taliban kuwazuia wanawake kusoma vyuo vikuu ni kinyume cha sheria za Kiislamu

Al-Azhar: Hatua ya Taliban kuwazuia wanawake kusoma vyuo vikuu ni kinyume cha sheria za Kiislamu

Sheikhe Mkuu wa Kituo cha Kiislamu cha Al-Azhar cha Misri ameutaka utawala wa Taliban kuondoa marufuku ya elimu ya juu kwa wanawake nchini Afghanistan. Sheikhe Mkuu wa Al-Azhar , Sheikh Ahmed El-Tayeb Al-Azhar amesema  amesikitishwa sana na uamuzi wa Taliban wa kuwapiga marufuku wanawake wa Afghanistan kutoendelea na masomo ya chuo kikuu. Katika taarifa yake…

Nchi za Kiislamu zalaani Taliban kuwazuia wanawake Afghanistan kusoma vyuo vikuu

Nchi za Kiislamu zalaani Taliban kuwazuia wanawake Afghanistan kusoma vyuo vikuu

Jumuiya ya Ushirikiano wa Nchi za Kiislamu (OIC) imebainisha masikitiko yake kuhusu uamuzi wa utawala wa Taliban nchini Afghanistan kuwapiga marufuku wanawake kuendelea na elimu katika vyuo vikuu nchini humo. OIC imesema katika taarifa yake kwamba Katibu Mkuu wa jumuiya Hissein Brahim Taha analaani hatua hiyo. Katibu mkuu na mjumbe wake maalum walikuwa wameonya dhidi…

Taliban yapiga marufuku masomo ya Chuo Kikuu kwa wanawake nchini Afghanistan

Taliban yapiga marufuku masomo ya Chuo Kikuu kwa wanawake nchini Afghanistan

Serikali ya Taliban imesitisha elimu ya Chuo Kikuu kwa wanafunzi wote wa kike nchini Afghanistan, hatua ya hivi karibuni kabisa ambayo inakosolewa huku kundi hilo likituhumiwa kwamba, linakandamiza haki na uhuru wa wanawake wa nchi hiyo. Msemaji wa Wizara ya Elimu ya Juu ya Afghanistan ameithibitisha kusitishwa kwa elimu ya ngazi ya Chuo Kikuu kwa…

Umoja wa Mataifa na kutotoa kiti kwa serikali ya Taliban

Umoja wa Mataifa na kutotoa kiti kwa serikali ya Taliban

Umoja wa Mataifa umepuuza na kutupilia mbali takwa la serikali ya Taliban na hivyo kwa mara nyingine tena kukikabidhi kiti cha uwakilishi wa Afghanistan katika umoja huo kwa Nasir Ahmad Faiq Mwakilishi wa Kudumu wa Afghanistan katika Umoja wa Mataifa. Katika hali ambayo serikali ya Taliban ilikuwa imemuarifisha Sohail Shaheen kwa ajili ya nafasi hiyo ili…

Sisitizo la kuchunguzwa jinai za jeshi la Marekani nchini Afghanistan

Sisitizo la kuchunguzwa jinai za jeshi la Marekani nchini Afghanistan

Sambamba na kuanza uchunguzi kuhusiana na jinai za kivita nchini Afghanistan unaofanywa na Mahakama ya Kimataifa ya Jinai (ICC), Shirika la Kutetea Haki za Binadamu la Human Rights Watch limetoa wito wa kuchunguzwa mashambulio ya mauaji ya jeshi la Marekani nchini Afghanistan. Katika ripoti yake ya hivi karibuni, Human Rights Watch imetangaza kuwa, katika miaka…

Kusambaratika miundombinu ya uchumi wa Afghanistan katika miaka 20 ya kukaliwa kwa mabavu na Marekani

Kusambaratika miundombinu ya uchumi wa Afghanistan katika miaka 20 ya kukaliwa kwa mabavu na Marekani

Waziri wa Uchumi wa serikali ya wanamgambo wa Taliban nchini Afghanistan amesema kuwa, miaka 20 ya kukaliwa kwa mabavu nchi hiyo na wanajeshi wa Marekani ndio sababu kuu ya kusambaratika miundombinu ya uchumi wa nchi hiyo. Qari Din Muhammad Hanif ameeleza kuwa, katika kipindi cha miaka 20 cha uwepo wa majeshi vamizi ya Marekani nchini…

Kukaribia kumalizika muhula wa serikali ya muda ya Taliban nchini Afghanistan

Kukaribia kumalizika muhula wa serikali ya muda ya Taliban nchini Afghanistan

Msemaji wa serikali ya muda ya Taliban nchini Afghanistan amesema kipindi cha uongozi wa serikali hiyo kitamalizika baada ya muda si mrefu ujao. Zabihullah Mujahid amevieleza vyombo vya habari katika mji mkuu wa nchi hiyo Kabul kwamba: juhudi mbalimbali zinaendelea kufanywa kwa ajili ya kupatikana mazingira mapya Afghanistan na serikali ya muda kuhitimisha shughuli zake. Mujahid…