UNICEF yaitaka serikali ya Taliban ifungue skuli zote za wasichana Afghanistan
Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto (UNICEF) limeitaka serikali ya Taliban inayotawala Afghanistan izifungue skuli zote za wasichana nchini humo. Baada ya kuingia madarakani Agosti 15, 2021, kundi la Taliban lilizifunga skuli za wasichana za ngazi ya kati na sekondari kwa lengo la kufanya baadhi ya mageuzi. Shirika la habari la Shafaqna Afghanistan…
Taliban: Hatuna mpango wa kuutambua rasmi utawala haramu wa Israel
Msemaji wa Ofisi ya Kisiasa ya Taliban nchini Qatar amesema kuwa, kundi hilo halina mpango wa kuutambua rasmi utawala haramuu wa Israel. Mulla Muhammad Naeem amekanusha taarifa za baadhi ya vyombo vya habari vinavyoeleza kwamba, kundi la Taliban halina tatizo na nchi yoyote ile ukiwemo utawala ghasibu wa Israel na kubainisha kwamba, amenukuliwa vibaya kwani huo…
Russia: Marekani irejeshe fedha za Afghanistan zilizoibwa
Mwakilishi wa Kudumu wa Russia katika Umoja wa Mataifa ameitaka Marekani izirejeshe fedha zilizoibiwa Afghanistan. Vasily Nebenzya ametoa mwito huo alipohutubia kikao cha Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa. Kwa mujibu wa shirika la habari la Russia TASS, mkutano wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa wa kujadili suala la Afghanistan uligeuka uwanja wa utoaji tuhuma…
Watu 180 waaga dunia kutokana na mafuriko nchini Afghanistan
Watu wasiopungua 180 wamefariki dunia nchini Afghanistan kutokana na mafuriko na matukio yanayohusiana na mvua kali zilizonyesha hivi karibuni. Msemaji wa serikali ya Taliban nchini humo, Zabihullah Mujahid amesema mbali na watu 182 kuaga dunia kwenye janga hilo la kimaumbile, wengine zaidi ya 250 wamejeruhiwa. Amesema nyumba zaidi ya 3,000 zimesombwa na maji ya mafuriko hayo na…
Mauaji ya Ayman al Zawahiri yapokewa kwa hisia tofauti
Mauaji ya Ayman al Zawahiri, kiongozi wa mtandao wa al Qaida katika operesheni ya droni iliyofanywa na wanajeshi wa Marekani, yamepokewa kwa hisia tofauti ya duru za kisiasa za nchi hiyo. Mapema leo asubuhi, rais wa Marekani, Joe Biden ametangaza habari ya kuuawa Ayman al Zawahiri katika shambulio la ndege isiyo na rubani lililofanywa na…
Wanawake wa Afghanistan wakosoa kutoalikwa katika kikao cha Loya Jirga
Wanawake wa Afghanistan wamekosoa kufanyika kikao cha maulamaa wa kidini wa Baraza la Ushauri kwa ajili ya amani ya Afghanistan (Loya Jiirga) bila ya wanawake wa nchi hiyo kuhudhuria. Kutoshirki wanawake katika kikao hicho kunamaanisha kupuuzwa nusu ya jamii ya watu wa Afghanistan. Kikao cha siku tatu cha faragha cha Loya Jirga kimefanyika Kabul mji…
255 wauawa na mamia wajeruhiwa katika tetemeko kubwa la ardhi lililoikumba Afghanistan
Watu wasiopungua 255 wameuawa na wengine zaidi ya 200 wamejeruhiwa baada ya tetemeko kubwa la ardhi kuyakumba maeneo ya mbali kusini mashariki ya Afghanistan na nchi jirani ya Pakistan alfajiri ya kuamkia leo. Mkuu wa wizara inayoshughulikia majanga ya kimaumbile katika serikali ya Taliban Mohammad Nassim Haqqani amesema, vifo vingi zaidi vimetokea katika mkoa wa…
Zaidi ya silimia 90 ya wananchi wa Afghanistan hawana chakula cha kutosha, WFP yatangaza
Shirika la Mpango wa Chakula la Umoja wa Mataifa (WFP) limetangaza kuwa, asilimia 95 ya wananchi wa Afghanistan hawana chakula cha kutosha. Taarifa yay Shirika la Mpango wa Chakula la Umoja wa Mataifa (WFP) kanda ya Asia-Pasific imeeleza kwamba, katika miezi ya hivi karibuni hali ya kibinadamu nchini Afghanistn imezidi kuwa mbaya na kwamba, idadi ya watu…