Mabadiliko ya hali ya hewa kusababisha mafuriko mabaya barani Afrika
Uchunguzi uliochapishwa na gazeti moja la Marekani umebaini kuwa kuna uwezekano wa kutokea mafuriko makubwa yatakayosababisha vifo vingi barani Afrika. Mtandao wa gazeti la Washington Post la Marekani umeripoti kuwa, watafiti wamefikia hitimisho kwamba mabadiliko ya hali ya hewa yanayosababishwa na binadamu yameongeza uwezekano wa kunyesha mvua kubwa kupita kiasi itakayosababisha mafuriko mara 80 zaidi…
WHO: Watu milioni 24 wanaishi na ugonjwa wa kisukari barani Afrika
Wakati jana Jumatatu ulimwengu uliadhimisha siku ya kisukari duniani, bara la Afrika linaonekana kuwa na changamoto kubwa ya ugonjwa huo kwa mujibu wa takwimu mpya za Shirika la Afya la Duniani (WHO). Maadhimisho hayo yanayofanyika kila mwaka kwa lengo la kuelimisha umma kuhusu ongezeko la mzigo wa ugonjwa huo na mikakati ya kuzuia na kudhibiti…
Bidhaa za Iran zinazidi kupata umaarufu barani Afrika
Kaimu Mkuu wa Kituo cha Biashara ya Iran na Afrika amesema: “Inatabiriwa kuwa kwa kasi ya sasa ya ustawi wa biashara ya Iran na Afrika katika mwaka huu (1401 Hijria Shamsia) kiwango cha mauzo ya bidhaa za Iran barani Afrika kitafika dola bilioni 1.8. Kwa mujibu wa Shirika la Habari la IRNA, Sayyid Ruhullah Latifi,…
Wakongo wafanya mandamano makubwa dhidi ya waasi wa M23 mjini Bukavu
Wananchi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo wenye hasira wamechoma moto bendera ya Umoja wa Ulaya katika mji wa Bukavu mashariki mwa nchi hiyo, huku mamia ya wakiandamana dhidi ya waasi wa M23. Wananchi hao wameeleza kutoridhishwa kwao na uingiliaji wa mataifa makubwa kama vile Marekani, Uingereza na Ufaransa katika masuala ya ndani ya nchi…
Matokeo ya Sensa: Idadi ya watu Tanzania yafikia milioni 61.74
Rais Samia Suluhu Hassan wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ametangaza matokeo ya Sensa ya Watu na Makazi iliyofanyika Agosti mwaka huu akisema kuwa idadi ya Watanzania ni milioni 61,741,120. Akitangaza matokeo hayo, Rais Samia amesema, kati yao wanawake ni milioni 31.6 sawa na asilimia 51 na wanaume milioni 30.53 sawa na asilimia 49 ya…
Afrika Kusini yaishambulia US kwa kutoa ‘tahadhari ya shambulio la kigaidi’
Viongozi wa Afrika Kusini wameikosoa serikali ya Marekani kwa kutoa tahadhari ya uwezekano wa kutokea shambulizi la kigaidi katika nchi hiyo ya kusini mwa Afrika. Jana Ijumaa, Idara ya Taifa ya Operesheni za Pamoja na Intelijensia ya Afrika Kusini (Natjoints) iliwaonya wananchi wa nchi hiyo ya kusini mwa Afrika dhidi ya kusambaza taarifa za uwongo…
Mawaziri wa Uganda waanza kujifunza Kiswahili
Mawaziri wa Uganda wameazimia kuanza kujifundisha lugha ya Kiswahili, ambayo mbali na kuwa lugha ya kitaifa, lakini pia ni lugha rasmi katika nchi hiyo ya Afrika Mashariki. Uganda hivi karibuni iliidhinisha Kiswahili kuwa lugha rasmi ya pili nchini humo baada ya Kiingereza, na kuifanya lugha hiyo kuwa ya lazima kufundishwa mashuleni. Makamu wa Kwanza wa…
Takwa la Umoja wa Afrika kwa Wamagharibi la kuamiliana kwa heshima na mataifa masikini
Kupamba moto vita vya Russia na Ukraine na kusambaa mgogoro wa kiuchumi katika akthari ya mataifa ya dunia, kumezifanya nchi za Kiafrika zitengwe na kutupwa mkono zaidi. Hali hii imezifanya nchi nyingi za bara hilo zikabiliwe na tatizo la kushindwa kujidhaminia mahitaji muhimu kama chakula na dawa. Kuhusiana na hilo, Rais wa Senegal, ambaye ndiye…