
Wapalestina wautaka Umoja wa Afrika kuiondoa Israel katika umoja huo
Viongozi na makundi ya ukombozi wa Palestina wameutaka Umoja wa Afrika (AU) kufikiria upya uamuzi wa mwaka jana wa kuipa Israel hadhi ya kuwa mwangalizi katika umoja huo. Wito huo wa pamoja umetolewa wakati wakuu wa nchi za Afrika wakikutana mjini Addis Ababa katika mkutano wa kilele wa siku mbili wa jumuiya hiyo yenye wanachama 55,…

Ujumbe wa ECOWAS na wanajeshi waliofanya mapinduzi nchini Burkina Faso
Baada ya kupita wiki moja tangu kutokea mapinduzi ya kijeshi nchini Burkina Faso, ujumbe wa makamanda wa jeshi wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Kiuchumi ya Nchi za Magharibi mwa Afrika (ECOWAS) upo katika nchi hiyo na umekutana na kufanya mazungumzo mjini Ouagadougou na wanachama wa Baraza la Utawala wa Kijeshi. Mazungumzo baina ya wanajeshi…

Katibu Mkuu wa UN alaani “janga la mapinduzi” baada ya Kabore kupinduliwa Burkina Faso
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres, amelaani kile alichokiita “janga la mapinduzi” ambalo ulimwengu unashuhudia, akieleza kuwa anafuatilia kwa wasiwasi mkubwa matukio ya sasa nchini Burkina Faso. Guterres ameeleza wasiwasi wake hasa kuhusu hatima na usalama wa Rais Roch Marc Christian Kabore wa Burkina Faso kufuatia mapinduzi yaliyofanywa na vikosi vya wanajeshi juzi Januari 23….

Shirika la Iran Khodro laanza tena kuunda magari Afrika
Shirika la Iran Khodro, ambalo ndilo shirika kubwa zaidi la kuunda magari Asia Magharibi, limetangaza kufungua tena kiwanda chake cha kuunda magari nchini Senegal. Shirika hilo la Iran litaanza kuunda magari aina ya Samand katika mji wa Thies, ambao ni wa pili kwa ukubwa Senegal na uko mbali wa kilimota 70 kutoka mji mkuu, Dakar….

Iran yasikitishwa na mauaji yaliyofanywa na magaidi Burkina Faso
Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran ametangaza kufungamana na familia za raia wa Burkina Faso ambao waliuawa katika hujuma ya kigaidi hivi karibuni. Katika taarifa leo Jumatatu, Saeed Khatibzadeh Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amebainisha masikitiko yake makubwa kutokana na kupoteza maisha raia wa Burkina Faso katika hujuma…

Tanzania yatangaza miradi ya kimkakati maonyesho Dubai
Dar es Salaam. Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara, Dotto James amesema Tanzania inatangaza miradi mikubwa ya kimkakati katika maonyesho ya kimataifa yanayofanyika Dubai katika Falme za Kiarabu (UAE). James ameyasema hayo leo Jumanne Oktoba 26 jijini Dar es Salaam wakati akitoa mrejesho wa ziara yake huko Dubai ambako alikwenda kuangalia ushiriki wa Tanzania…