#afrika_kusini

Kwa mara ya kwanza nchini Afrika Kusini, Muislamu awa Meya wa Jiji la Johannesburg

Kwa mara ya kwanza nchini Afrika Kusini, Muislamu awa Meya wa Jiji la Johannesburg

Kwa mara ya kwanza katika historia ya Afrika Kusini, diwani Muislamu kutoka chama kidogo cha Al Jama-ah amechagualiwa kuwa Meya wa Jiji la Johannesburg, kitovu cha biashara cha nchi hiyo. Thapelo Amad, amepigiwa kura na baraza la jiji kuchukua nafasi ya meya Mpho Phalatse, mwanachama wa chama kikuu cha upinzani nchini Afrika Kusini, Democratic Alliance…

Afrika Kusini yatetea uamuzi wake kuhusu mazoezi ya kijeshi na Russia na China

Afrika Kusini yatetea uamuzi wake kuhusu mazoezi ya kijeshi na Russia na China

Waziri wa Mambo ya Nje wa Afrika Kusini ametetea uamuzi wa nchi yake wa kufanya mazoezi ya pamoja ya jeshi la majini kati yake na nchi kubwa za Russia na China mwezi ujao wa Februari katika pwani yake ya mashariki mwa nchni hiyo ya kusini mwa Afrika. Afrika Kusini ni mwanachama wa BRICS, kambi ya…

Mashindano ya Kitaifa ya Qur’ani Tukufu Afrika Kusini yafanyika Pretoria

Mashindano ya Kitaifa ya Qur’ani Tukufu Afrika Kusini yafanyika Pretoria

Toleo la 13 la mashindano ya kitaifa ya Qur’ani Tukufu nchini Afrika Kusini yalifanyika katika mji mkuu, Pretoria. Baraza la Taifa la Qur’ani la Afrika Kusini (SANQC) liliandaa hafla hiyo iliyohudhuriwa na wahifadhi wa Qur’ani kutoka kote katika nchi hiyo. Mashindano hayo yalifanyika katika Msikiti wa Nour wa Pretoria ambapo Imamu na mhubiri wa Msikiti…

Idadi ya vifo katika mkasa wa mlipuko wa lori la kubeba gesi Afrika Kusini yafikia 34

Idadi ya vifo katika mkasa wa mlipuko wa lori la kubeba gesi Afrika Kusini yafikia 34

Wizara ya Afya ya Afrika Kusini imetangaza kuwa, idadi ya watu walioaga dunia katika mlipuko wa lori la kubeba gesi uliotokea Jumamosi iliyopita jirani na mji wa Johannesburg imeongezeka na kufikia wahanga 34. Taarifa ya Wizara ya Afya ya Afrika Kusini imeeleza kuwa, miongoni mwa walioaga dunia wamo wapita njia ambao walikuwa karibu na tukio…

Makumi ya maiti za wachimba migodi ‘haramu’ zapatikana Afrika Kusini

Makumi ya maiti za wachimba migodi ‘haramu’ zapatikana Afrika Kusini

Polisi ya Afrika Kusini inachunguza kisa cha kugunduliwa makumi ya maiti za watu wanaoshukiwa kuwa wachimba migodi ‘haramu’ katika mji wa Krugersdorp, magharibi mwa jiji la Johannesburg. Msemaji wa Polisi ya Afrika Kusini, Brenda Muridili  amesema waliopoa maiti 19 kwenye mgodi binafsi katika mji huo hapo jana, huku miili mingine miwili ikigunguliwa mapema leo Alkhamisi. Jeshi…

Afrika Kusini yaishambulia US kwa kutoa ‘tahadhari ya shambulio la kigaidi’

Afrika Kusini yaishambulia US kwa kutoa ‘tahadhari ya shambulio la kigaidi’

Viongozi wa Afrika Kusini wameikosoa serikali ya Marekani kwa kutoa tahadhari ya uwezekano wa kutokea shambulizi la kigaidi katika nchi hiyo ya kusini mwa Afrika. Jana Ijumaa, Idara ya Taifa ya Operesheni za Pamoja na Intelijensia ya Afrika Kusini (Natjoints) iliwaonya wananchi wa nchi hiyo ya kusini mwa Afrika dhidi ya kusambaza taarifa za uwongo…

Rais wa Afrika Kusini, Cyril Ramaphosa ameilaumu NATO kwa vita vya Russia nchini Ukraine

Rais wa Afrika Kusini, Cyril Ramaphosa ameilaumu NATO kwa vita vya Russia nchini Ukraine

Rais wa Afrika Kusini, Cyril Ramaphosa, ameilaumu NATO kwa vita vya Ukraine na kusema kuwa atapinga wito wa kuilaani Russia. Matamshi haya ya Ramaphosa yanatia shaka iwapo atakubaliwa na Ukraine au nchi za Magharibi kama mpatanishi katika mzozo huo. Ramaphosa ambaye alikuwa akizungumza bungeni, amesema: “Vita hivyo vingeweza kuepukika kama NATO ingezingatia maonyo kutoka kwa viongozi…

Waziri wa Mambo ya Nje wa Afrika Kusini: Hivi karibuni tutachukua hatua dhidi ya ubaguzi wa rangi wa Israel

Waziri wa Mambo ya Nje wa Afrika Kusini: Hivi karibuni tutachukua hatua dhidi ya ubaguzi wa rangi wa Israel

Faraan : Waziri wa Mambo ya Nje wa Afrika Kusini alikosoa vikali utawala huo ghasibu na ubaguzi wake wa rangi dhidi ya Wapalestina. Kulingana na Fars News Agency International Group; Waziri wa Mambo ya Nje wa Afrika Kusini Nalidi Bandur katika hotuba yake mbele ya bunge aliukosoa utawala wa Kizayuni wa Israel kwa uvamizi wake…