Dodoma. Serikali imetangaza tena ajira 736 za kada ya afya zilizokosa waombaji wenye sifa huku wengi wakiwa ni wauguzi ngazi ya cheti. Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tamisemi, Innocent Bashungwa ametoa taarifa hiyo leo Jumapili Juni 26,2022 wakati akitangaza waliochaguliwa katika ajira mpya zilizotangazwa na serikali mapema Aprili, 2022 mbapo walimu 9800 wamepatikana. Kwa upande…