Polisi ya Kimataifa, INTERPOL, imetoa kibali cha kimataifa cha kukamatwa kwa bilionea wa Angola na bintiye rais wa zamani wa nchi hiyo Isabel dos Santos. Shirika la habari la Lusa la Ureno, likinukuu duru rasmi, limesema kibali cha INTERPOL kilitolewa baada ya waendesha mashtaka wa Angola kuliomba shirika hilo “kumtafuta, kumkamata” na kumrejesha dos Santos….