
Upinzani Bahrain waafikiana kususia uchaguzi wa leo wa Bunge
Vyama na makundi ya upinzani nchini Bahrain yameafikiana kwa kauli moja juu ya kuususia uchaguzi wa Bunge unaotazamiwa kufanyika hii leo nchini humo. Naibu Katibu Mkuu wa mrengo mkubwa zaidi wa upinzani nchini humo wa al-Wefaq ametangaza kuwa, makundi yote ya upinzani katika nchi hiyo ndogo ya Ghuba ya Uajemi yameafikiana kususia uchaguzi huo wa leo….

Sheikh Isa Qassim: Uchaguzi ujao unalenga kuimarisha udikteta Bahrain
Kiongozi mashuhuri wa kidini nchini Bahrain amesema uchaguzi ujao wa Bunge nchini humo hauna lengo jingine isipokuwa kuimarisha mienendo ya kiimla na kidikteta ya watawala wa Aal-Khalifa. Sheikh Isa Qassim, kiongozi wa kidini wa mapinduzi ya Bahrain amesema hayo katika ujumbe aliotuma kwenye mtandao wa kijamii wa Twitter hapo jana na kuongeza kuwa: Chaguzi nchini…

Wanazuoni wa Bahrain wanaosota jela: Tunatumai Papa Francis atazungumza neno la haki
Wanazuoni wa Bahrain wanaosota kwenye jela za utawala wa kifalme wa nchi hiyo wa ukoo wa Aal Khhalifa wameeleza katika taarifa waliyotoa kumhutubu Kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani Papa Francis kwamba, wanatumai kiongozi huyo wa kidini atasema ukweli na kuitikia wito wa imani katika ziara yake ijayo huko Bahrain. Shirika la habari la IRNA limeripoti…

Bahrain inaongoza kwa idadi ya wafungwa wa kisiasa Uarabuni
Kituo cha Haki za Binadamu cha Bahrain (BCHR) kimesema Bahrain inaongoza kwa kuwa na idadi kubwa zaidi ya wafungwa wa kisiasa miongoni mwa nchi zote za Kiarabu. Taarifa ya asasi hiyo ya kutetea haki za binadamu Bahrain imesema vyombo vya usalama vya utawala wa Manama vinawashikilia wafungwa wa kisiasa zaidi ya 4,500 katika jela mbalimbali za nchi…

Jumuiya ya al-Wifaq: Uchaguzi ujao wa Bunge Bahrain ni wa kuimarisha dhulma
Jumuiya ya Kitaifa na Kiislamu nchini Bahrain ya Al-Wifaq imetangaza kuwa, uchaguzi ujao wa Bunge nchini humo ni wenzo na chombo cha kuimarisha dhulma na kuendelea ufisadi Hayo yameelezwa na Sheikh Hussein al-Daihi, Naibu Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Kitaifa na Kiislamu nchini Bahrain ya Al-Wifaq ambaye amesisitiza kuwa, ”kubakia mgogoro wa kisiasa na hali ya…

Sheikh Issa Qassim: Kujengwa kitongoji cha walowezi wa Kiyahudi Manama ni jinai
Kiongozi wa Harakati ya Kiislamu ya Bahrain amekosoa viikali uamuzi wa utawala wa Aal Khalifa wa kuanzisha kitongoji cha walowezi wa Kiyahudi katika mji mkuu Manama na kueleza kwamba, hatua hiyo ni jinai na dhulma ya wazi dhidi ya wananchi wa nchi hiyo ya Kiarabu. Sheikh Issa Qassim, kiongozi wa kimaanawi wa Mapinduzi ya Wananchi wa…

Mfalme wa Bahrain amuuzulu waziri wake kwa kukataa kumpa mkono balozi wa Israel
Mfalme wa Bahrain amemuuzulu waziri mwanamke wa nchi hiyo kwa kukataa kumpa mkono balozi wa utawala wa Kizayuni wa Israel wa mjini Manama na kwa kupinga hatua ya kuanzisha ya uhusiano wa kawaida na utawala huo haramu. Tovuti ya habari ya Shahab News imeripoti kuwa, hivi karibuni ilifanyika hafla katika makazi ya balozi wa Marekani…

Sheikh Isa Qasim atoa wito kwa watu kupinga uchaguzi wa kikatili nchini Bahrain
Huku akiutaja uchaguzi wa nchi hii kuwa wa kikatili, kiongozi wa kiroho wa mapinduzi ya Bahrain amewataka wananchi wa Bahrain wasikae kimya mbele ya chaguzi hizo. Kwa mujibu wa ripoti ya Shirika la Habari la Kimataifa la Fars, Sheikh Isa Qassem, kiongozi wa kiroho wa mapinduzi ya Bahrain siku ya Alkhamisi katika taarifa yake ya…