Pele, mchezaji mashuhuri wa soka wa Brazil ambaye anatajwa kuwa mwanasoka bora zaidi katika historia, ameaga dunia. Edson Arantes do Nascimento almaarufu Pele, alfariki dunia akiwa na umri wa miaka 82, familia yake imetangaza Alhamisi. Hospitali ya Albert Einstein iliyoko mjini Sao Paulo, ambako Pele alikuwa akipokea matibabu, imesema gwiji huyo wa kandanda alifariki saa…