
Paris yamwita nyumbani balozi wake baada ya wanajeshi wake kutimuliwa Burkina Faso
Baada ya serikali ya Burkina Faso kuiamuru Ufaransa iondoe wanajeshi wake katika kipindi cha mwezi mmoja ujao, mkoloni huyo kizee wa Ulaya amehamakishwa na hatua hiyo na ameamua kumrudisha nyumbani balozi wake kutoka Ouagadougou. Kwa mujibu wa ripoti ya Shirika la Habari la Kimataifa la Fars, siku moja baada ya Ufaransa kusema kuwa itaheshimu uamuzi…

Mkoloni kizee Mfaransa atimuliwa rasmi nchini Burkina Faso
Serikali ya Burkina Faso imeamua kusitisha mkataba wa kijeshi ulioruhusu wanajeshi wa Ufaransa wafanye wanalotaka nchini humo. Mkataba huo wa kijeshi ulikuwa umeipa nchi ya Ulaya ya Ufaransa haki kubwa kuliko hata raia wenyewe wa Burkina Faso. Ufaransa hivi sasa ina wanajeshi wake maalumu 400 katika nchi ya Afrika Magharibi. Serikali mpya ya Burkina Faso imesema,…

Ufaransa yatakiwa iondoe jeshi lake Burkina Faso haraka iwezekavyo
Serikali ya kijeshi inayotawala Burkina Faso imeitaka Ufaransa iwaondoe wanajeshi wake katika nchi hiyo ya Afrika Magharibi katika kipindi kifupi kijacho. Chanzo cha habari ndani ya serikali hiyo kimenukuliwa na shirika la habari la Reuters kikisema kuwa, wanajeshi hao wa Ufaransa wametakiwa wawe wameondoka kikamilifu nchini Burkina Faso ndani ya mwezi mmoja ujao. Haya yanajiri baada…

Takriban wanawake 50 waliotekwa nyara nchini Burkina Faso wapatikana
Vyombo vya habari vimetangaza kuwa, takriban wanawake 50 waliotekwa nyara hivi majuzi kaskazini mwa Burkina Faso na watu wanaoshukiwa kuwa magaidi, wamepatikana. Shirika la habari la Burkina Faso limeripoti habari hiyo kwa kuandika: “Wanawake waliotekwa nyara na magaidi usiku wa tarehe 12-13 mwezi huu wa Januari 2023 huko Arbinda wamepatikana.” Shirika la Habari la Taifa…

Waandamanaji wenye hasira wajaribu kuvamia ubalozi wa Ufaransa nchini Burkina Faso
Polisi nchini Burkina Faso walirusha mabomu ya kutoa machozi siku ya Ijumaa kuwatawanya waandamanaji waliokuwa na hasira waliojaribu kuvamia ubalozi wa Ufaransa katika mji mkuu Ouagadougou, vyombo vya habari vya ndani vimeripoti. Waandamanaji hao waliokuwa wakitaka balozi wa Ufaransa nchini humo atimuliwe, walikusanyika katika uwanja wa manispaa asubuhi kabla ya kuelekea kwenye ubalozi wa Ufaransa,…

Makumi ya magaidi wakufurishaji waangamizwa nchini Burkina Faso
Jeshi la Burkina Faso limetangaza kuwa, limeangamiza magaidi 100 wakufurishaji katika operesheni za kijeshi lilizofanya kwa nyakati tofauti katika nchi hiyo ya magharibi mwa Afrika. Shirika la habari la Tasnim limenukuu taarifa ya jeshi la Burkina Faso ikitoa ufafanuzi kwa kusema, operesheni zilizoangamiza magaidi hao 100 wakufurishaji zimefanyika kwenye maeneo mbalimbali na kwa nyakati tofauti…