#Ghana

Ghana kuipiga kando dola ya Marekani katika ununuzi wa mafuta

Ghana kuipiga kando dola ya Marekani katika ununuzi wa mafuta

Serikali ya Ghana inaanda sera mpya ya kununua bidhaa za mafuta kwa kutumia dhahabu badala ya sarafu ya dola ya Marekani. Makamu wa Rais wa Ghana, Mahamudu Bawumia amesema katika ujumbe alioutuma kwenye mtandao wa Facebook kuwa: Iwapo mpango huu utatekelezwa barabara kama ilivyopangwa katika robo ya kwanza ya mwaka 2023, tutabadilisha mlingano wa mbinu za malipo…