Harakati za Hamas, Jihad Islami zalaani vikali ziara ya rais wa Israel nchini Bahrain
Harakati mbili za mapambano ya Kiislamu (muqawama) Palestina za Hamas na Jihad Islami zenye makao yake katika Ukanda wa Gaza zimelaani vikali ziara inayoendelea nchini Bahrain ya rais wa utawala ghasibu wa Israel. Afisa mwandamizi wa Hamas Basim Naim na msemaji wa Jihad Islami Tariq Salmi walilaani safari hiyo siku ya Jumapili saa chache baada…
Ismail Ridhwan: Jinai ya kumuua shahidi Ammar Mefleh haitasalia bila jibu
Afisa wa ngazi ya juu wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (Hamas) ameeleza kuwa, jinai ya kumuua shahidi Ammar Mefleh ni jinai ya kivita na dhidi ya binadamu na haitasalia bila jibu. Mwanajeshi wa utawala ghasibu wa Israel juzi Ijumaa alikabiliwa na muqawama wakati alipojaribu kumtia nguvuni Ammar Mefleh katika kitongoji cha Huwara…
Hamas: Wavamizi watateketea katika moto wa hujuma dhidi ya Msikiti wa Al-Aqsa
Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (Hamas) imewatahadharisha Wazayuni kuhusu kuendelea kuuhujumu Msikiti wa al Aqsa na kuwatolea mwito Wapalestina kuhudhuria kwa nguvu zote na kwa mshikamano katika msikiti huo. Msikiti wa al Aqsa ambao ni nembo kuu ya utambulisho wa Kiislamu na wa Palestina katika mji wa Baitul Muqaddas umekuwa ukilengwa na kukabiliwa…
Mzayuni Ben-Gvir asema ataushambulia msikiti wa al Aqsa, HAMAS yamjibu kuwa atashindwa!
Itamar Ben-Gvir, mzayuni mwenye misimamo ya kufurutu mpaka na kiongozi wa chama cha Nguvu ya Kiyahudi ambaye amependekezwa kuwa waziri wa usalama wa ndani katika baraza la mawaziri la Benjamin Netanyahu, ametangaza kuwa, mnamo siku chache zijazo ataushambulia Msikiti wa Al-Aqsa. Kwa mujibu wa tovuti ya Falastin Al-Yum, Ben-Gvir, amesisitiza katika mahojiano ya televisheni akisema:…
Hamas: Mpango wa wavamizi wa Kizayuni huko al Khalil utashindwa
Sambamba na kupongeza muqawama na mapambano ya wananchi dhidi ya utawala ghasibu wa Israel, msemaji wa harakati ya Hamas amesisitiza kuwa, juhudi za utawala wa Kizayuni za kuimarisha ujenzi wa vitongoji vya walowezi huko al Khalil hazitafanikiwa. Hali ya sasa katika ardhi zinazokaliwa kwa mabavu hususan katika Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan ni tata mno, ambapo…
HAMAS: Msikiti wa Aqsa uko chini ya dhulma kubwa ya Wazayuni
Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina HAMAS imesema kuwa, Msikiti wa al Aqsa (ambao ni Kibla cha Kwanza cha Waislamu) ni miongoni mwa nembo kuu ya Uislamu na kwamba mji mtakatifu wa Quds uliko Msikiti huo mtakatifu, daima umekuwa ukilengwa na maadui Wazayuni. Ayad Fannunah, mmoja wa viongozi wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu…
Ujumbe wa HAMAS waonana na Rais wa Syria mara ya kwanza baada ya miaka 10
Duru za Syria zimetangaza habari ya kukutana ujumbe mmoja wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina HAMAS na Rais Bashar al Assad wa nchi hiyo ikiwa ni mara ya kwanza katika kipindi cha miaka 10 iliyopita. Televisheni ya al Mayadeen ilitangaza habari hiyo jana Jumatano na kuzinukuu duru hizo zikisema kuwa, ujuumbe wa Palestina…
HAMAS na Jihadul-Islami: Jinai za Israel hazina taathira yoyote kwa azma ya taifa la Palestina
Harakati za Hamas na Jihadul Islami za Palestina zimesisitiza kuwa, Jinai za Israel hazina taathira yoyote kwa irada na azma ya taifa la Palestina na kwamba, Wapalestina wanafungamana kikamilifu na chaguo la muqawama na mapambano dhidi ya utawala ghasibu wa Israel. Taarifa ya Harakati za Hamas na Jihadul Islami za Palestina imetolewa kufuatia tukio la kuuawa…