#iran

Hamas yaishukuru Iran kwa kuunga mkono ukombozi wa Palestina

Hamas yaishukuru Iran kwa kuunga mkono ukombozi wa Palestina

Afisa mwandamizi wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina, Hamas, ameishukuru Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kwa kuunga mkono harakati za ukombozi wa Palestina. Mahmoud al-Zahar ameyasema hayo Jumatatu katika mahojiano na Radio ya Al Aqsa. Amesema Iran imekuwa ikiunga mkono harakati dhidi ya utawala wa Kizayuni wa Israel ambao unakalia kwa mabavu ardhi…

Ibrahim Raeisi: Hakuna mazungumzo yoyote yatakayoifanya Iran ilegeze msimamo katika haki zake

Ibrahim Raeisi: Hakuna mazungumzo yoyote yatakayoifanya Iran ilegeze msimamo katika haki zake

Rais Ibrahim Raeisi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, hakuna kikao au mazungumzo yoyote yale ambayo yatalifanya taifa hili lilegeze kamba na kufumbia macho haki zake. Rais wa Iran amesema hayo leo katika mkutano wa 17 wa Siku ya Kimataifa ya Msikiti na kueleza kwamba, serikali inafanya kila iwezalo na kwa nguvu zake…

Kufanyika kikao cha Kamisheni ya Pamoja ya Kiuchumi ya Iran na Pakistan mjini Islamabad

Kufanyika kikao cha Kamisheni ya Pamoja ya Kiuchumi ya Iran na Pakistan mjini Islamabad

Kikao cha 21 cha Kamisheni ya Pamoja ya Kiuchumi ya Iran na Pakistan kilianza Jumatano ya jana katika mji mkuu wa Pakistan Islamabad ambapo ujumbe wa Iran katika kikao hicho unaongozwa na Rostam Qassemi, Waziri wa Barabara na Ujenzi wa Miji. Katika kikao cha ufunguzi jana asubuhi, maafisa wa Iran na Pakistan walibainisha uhusiano mzuri…

Iran: Muqawama wa Kiislamu hauishii tu katika ukanda wa Asia Magharibi

Iran: Muqawama wa Kiislamu hauishii tu katika ukanda wa Asia Magharibi

Msemaji wa serikali ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, muqawama na mapambano ya Kiislamu si kitu cha kuishia kwenye eneo moja tu. Kwa mujibu wa shirika la habari la IRNA,  Ali Bahadori Jahromi alisema hayo jana kupitia mtandao wa kijamii wa Instagram kwa mnasaba wa tarehe 23 Mordad kwa kalenda ya Kiirani ya…

Iran yaitaka Marekani kukubali matakwa halali ya Jamhuri ya Kiislamu

Iran yaitaka Marekani kukubali matakwa halali ya Jamhuri ya Kiislamu

Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran Hossein Amir-Abdollahian ameitaka Marekani kuandaa mazingira ya kuafikiwa rasimu ya mwisho ya makubaliano ya mazungumzo ya Vienna kwa kukubali “matakwa halali” ya Jamhuri ya Kiislamu. Amir-Abdollahian aliyasema hayo Jumatano jioni katika manzungumzo na mwenzake wa Uturuki Mevlut Cavosoglu na kuongeza kuwa: “Tumefikisha ujumbe wetu kwa Marekani kupitia nchi…

Marekani yatiwa kiwewe na hatua ya Iran kurusha satalaiti anga za mbali

Marekani yatiwa kiwewe na hatua ya Iran kurusha satalaiti anga za mbali

Marekani imeghadhabishwa na hatua ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ya kurusha satalaiti katika anga za mbali kwa mafanikio, kwa kutumia roketi la Russia. Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani amesema katika taarifa kuwa, kitendo cha Russia cha kupanua uhusiano na ushirikiano na Iran kinapaswa kutazamwa na dunia kama tishio kubwa. Maafisa…

Sayyid Nasrullah: Iran ndio moyo wa Uislamu na mrengo wa muqawama

Sayyid Nasrullah: Iran ndio moyo wa Uislamu na mrengo wa muqawama

Katibu Mkuu wa Harakati ya Hizbullah ya Lebanon amesema Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ndio moyo wa Uislamu na mrengo wa muqawama wa Kiislamu duniani. Sayyid Hassan Nasrullah alisema hayo jana Jumanne mjini Beirut akiuhutubia umati wa waombolezaji wa Ashura ya Imam Hussein (AS) na kuongeza kuwa, Iran chini ya uongozi wa Ayatullah Ali Khamenei, Kiongozi Muadhamu…

Kiongozi Muadhamu ashiriki katika maombolezo ya Tasua ya Imam Husain AS

Kiongozi Muadhamu ashiriki katika maombolezo ya Tasua ya Imam Husain AS

Usiku wa kuamkia leo umesadifiana na usiku wa mwezi tisa Mfunguo Nne, Muharram, siku ambayo ni maarufu kwa jina la Tasua ya Imam Husain AS. Maombolezo ya usiku wa kuamkia leo yamefanyika katika kona zote za Iran na nje ya Iran ikiwemo Husainia ya Imam Khomeini MA mjini Tehran na kuhudhuriwa na Kiongozi Muadhamu wa…