
Jen. Shekarchi: Marekani, Israel zinajua vyema gharama ya kuitishia Iran
Msemaji wa Vikosi vya Ulinzi vya Iran amesema Marekani na utawala wa Kizayuni wa Israel zinatambua vizuri kile ambacho kitawafika iwapo zitathubutu kutelekeza kivitendo vitisho vyao dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu. Brigedia Jenerali Abolfazl Shekarchi, Msemaji wa Jeshi la Iran amesema ukongwe wa Rais Joe Biden na tabia yake ya kupenda kulala ndiyo imempelekea atumie lugha…

Iran: Israel ndio mzizi wa ugaidi na ukosefu wa usalama Asia Magharibi
Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema utawala wa Kizayuni wa Israel ndio chimbuko la vitendo vya kigaidi na ukosefu wa usalama na uthabiti katika eneo hili la Asia Magharibi. Naser Kan’ani alisema hayo jana Jumanne na kuongeza kuwa, hatua ya Marekani kuukingia kifua na kuunga mkono utawala…

Iran, Russia na China kushiriki katika mazoezi ya kijeshi Amerika ya Kusini
Iran, Russia na China zinapanga kushiriki katika mazoezi ya kijeshi yatakayoandaliwa na Venezuela ili kuonyesho nguvu zao kwa Marekani. Maneva hayo ya kijeshi yanafuatia yale yaliyoandaliwa na Iran yakishirikisha majeshi ya majini ya China na Russia kwa anwani ya “Ukanda wa Amani wa Baharini 2022” katika eneo la kaskazini mwa Bahari ya Hindi. Mazoezi mbalimbali ya kimbinu…

Iran na Uganda kuimarisha uhusiano wa kiuchumi
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran Anayehusika na Diplomasia ya Uchumi amekutana na kuzungumza kwa nyakati tofauti na Rais na Waziri Mkuu wa Uganda kwa lengo la kuimarisha uhusiano wa kiuchumi kati ya nchi mbili. Mahdi Safari amekutana na Waziri Mkuu wa Uganda Robinah Nabbanja na kujadili kuendeleza ushirikiano kati ya nchi mbili…

Marekani yatangaza vikwazo vipya dhidi ya sekta ya mafuta ya Iran
Wizara ya Fedha ya Marekani imeendeleza uraibu wa nchi hiyo wa kuziwekea vikwazo nchi mbalimbali kwa kutangaza vikwazo vipya dhidi ya sekta ya mafuta na petrokemikali ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran. Wizara ya Hazina ya Marekani jana Jumatano ilitangaza kuziwekea vikwazo kampuni mbalimbali zenye makao yao katika Umoja wa Falme za Kiarabu, eti kwa kufanikisha…

Rais wa Iran: Kuimarisha mabadilishano ya kibiashara na nchi za eneo ni dharura
Rais Ebrahim Raisi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuna udharura wa kutumia fursa zilizojitokeza kuimarisha uhususiano wa kibiashara na nchi za eneo. Rais Ebrahim Raeisi ameyasema hayo leo Jumatano mjini Tehran katika kikao cha Baraza la Mawaziri na kuongeza kuwa kuna udharura wa kuimarisha mabadilishano ya kibiashara na nchi za eneo hasa nchi…

Amir-Abdollahian: Mazungumzo yenye tija yanahitaji Marekani kuwa na nia ya dhati na kuwa tayari kubadilika
Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran Hossein Amir-Abdollahian amesema, mazungumzo yenye tija yanategemea upande wa Marekani utakavyokuwa na nia ya dhati, ubunifu na kuwa tayari kubadilika. Amir-Abdollahian ameyasema hayo katika mazungumzo aliyofanya Jumatatu kwa njia ya simu na Waziri wa Mambo ya Nje wa Oman Sayyid Badr Albusaidi ambapo sambamba na…

Ujumbe wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran kuhusu jinai za Marekani
Wizara ya Mambo ya Nje ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imetoa ujumbe wa Twitter kwa mnasaba wa kukumbuka jinai ya meli ya kivita ya Marekani iliyotungua ndege ya abiria ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika Ghuba ya Uajemi. Ujumbe huo umeambataisha taarifa za jinai hiyo ya kuogofya na kuwaenzi waliouawa shahidi katika tukio…