
Mabadilishano ya kibiashara baina ya Iran na Tanzania yameongezeka kwa 120%
Balozi mdogo wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran nchini Tanzania amesema, mabadilishano ya kibiashara kati ya nchi hizo mbili katika mwaka uliopita yaliongezeka kwa asilimia 120. Hossein Alvandi ameyasema hayo katika kikao cha wawakilishi wa vyama vya wafanyabiashara wa Iran na Tanzania kilichofanyika kwa njia ya intaneti na akaongezea kwa kusema, kuna fursa na mazingira…

Iran iko tayari kusaidia utatuzi wa kidiplomasia wa mzozo wa Ukraine
Iran imesisitiza dhamira yake ya kuchangia katika utatuzi wa kidiplomasia wa mzozo unaotokota nchini Ukraine, ambao sasa unaingia mwezi wa tano. Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran Hossein Amir-Abdollahian katika mazungumzo ya simu na mwenzake wa Ukraine Dmytro Kuleba ameashiria msimamo wa Iran wa kupinga vita na kusisitiza juu ya kutatuliwa mgogoro huo kwa njia…

China yaitaka Marekani kurekebisha makosa yake mkabala wa Iran
Kwa mujibu wa shirika la habari la Fars, Wizara ya Mambo ya Nchi za Nje ya China imesema kuwa Washington, ikiwa ni mwanzilishi wa mgogoro wa nyuklia wa Iran, inapaswa kurekebisha makosa yake na kujibu wasiwasi wa Tehran. Beijing imekuwa ikiilaumu Marekani mara kwa mara kwa hali ya sasa ya miradi ya kuzalisha nishati ya…

Raisi: Uwepo wa utawala wa Kizayuni unadhoofisha usalama wa eneo
Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema uwepo wa utawala wa Kizayuni wa Israel unaibua taharuki na kudhoofisha usalama wa eneo hili la Asia Magharibi. Rais wa Iran, Sayyid Ebrahim Raisi alisema hayo jana Jumatano katika kikao na mwenzake wa Azerbaijan, Ilham Aliyev, pambizoni mwa Mkutano wa 6 wa Nchi Zinazopakana na Bahari ya Kaspi huko Ashgabat,…

Raisi: Jamhuri ya Kiislamu ya Iran inaitambua Bahari ya Kaspi kuwa bahari ya amani na urafiki
Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema katika Mkutano wa Sita wa Nchi za Pwani mwa Bahari ya Kaspi kuwa: Iran inaitambua bahari hiyo kuwa ni bahari ya amani na urafiki na kiunganishi cha watu wa eneo hili. Sayyid Ebrahim Raisi amesisitiza kuwa Iran iko tayari kwa ajili ya ushirikiano wa pande zote kwa…

Ebrahim Raisi akutana na Vladimir Putin, Ashgabat
Rais Ebrahim Raisi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran leo anakutanza na mwenzake wa Russia Vladimir Putin katika kikao kitakachofanyika katika mji mkuu wa Turkmenistan, Ashgabat. Kwa mujibu wa taarifa mshauri wa rais wa Russia katika sera za kigeni Yuri Viktorovich Ushakov amesema Rais Putin leo atashiriki katika kikao cha viongozi wa Nchi za Pwani ya…

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi: Ushindi ndio matokeo ya kusimama kidete mbele ya maadui
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amehutubia kikao cha Mkuu wa Idara ya Mahakama ya Iran na maafisa na wafanyakazi wa chombo hicho akisema matokeo ya kusimama kidete mbele ya maadui ni kupata ushindi na maendeleo. Katika kikao hicho, Ayatullah Ali Khamenei amefafanua kanuni zisizobadilika za Mwenyezi Mungu katika jamii na kusema: Sababu ya ushindi wa kustaajabisha…

Indhari ya Waziri wa Usalama wa Iran: Magaidi hawatabakia salama
Waziri wa Usalama wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema magaidi wenye makao yao Albania hawatabakia salama kutokana na moto wa ulipizaji kisasi wa jinai walizotenda. Kundi la kigaidi la Munafikina (MKO) limehusika katika mauaji ya Wairani zaidi ya elfu 17, wakiwemo wabunge, maafisa wa ngazi za juu wa kiserikali na kijeshi, raia wa kawaida…