
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi: Shari bila shaka itasamabratishwa
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Sayyid Ali Khamenei amesema lengo kuu la wachochezi wa machafuko ya hivi karibuni ni kuliingiza taifa la Iran katika medani na kuongeza kuwa: “Mchafuko hayo bila shaka yatakomeshwa na taifa kuendelea kusonga mbele kwa nguvu zaidi na ari mpya katika uwanja wa maendeleo ya nchi.” Kwa mujibu wa…

Haki za taifa la Iran zimekiukwa kwa vikwazo vya Marekani dhidi ya IRIB, Press TV
Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran, Nasser Kan’ani, amelaani uamuzi wa hivi karibuni wa Marekani wa vikwazo vinavyolenga Shirika la Utangazaji la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran (IRIB) na Televisheni ya Press TV akisema ni ukiukaji wa haki za taifa la Iran. Katika ujumbe kupitia Twitter siku ya Ijumaa, Kan’ani amesema vikwazo…

Vikwazo vipya vya Umoja wa Ulaya na Uingereza dhidi ya Iran; mkinzano wa vitendo na kaulimbiu
Jumatatu ya jana tarehe 14 Novemba, Umoja wa Ulaya na Uingereza zilitangaza kuiwekea vikwazo vipya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika hatua iliyopangwa na kuratibiwa baina ya pande mbili hizo. Uingereza imetangaza kuwaweka katika orodha yake ya vikwazo watu na taasisi 24 za Kiirani kwa kisingizio cha kile kilichoelezwa kuwa kukiuka haki za binadamu. Hatua…

Iran yalaani shambulio la kigaidi la Istanbul Uturuki
Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran mapema leo alfajiri amelaani shambulio la kigaidi lililotokea jana jioni mjini Istanbul Uturuki na kuua na kujeruhi makumi ya watu. Kwa mujibu wa shirika la habari la IRNA, Nasser Kan’ani amesema, Tehran inalaani kitendo chochote cha kigaidi ambacho kinahatarisha usalama wa nchi na wananchi wa Uturuki….

Jenerali Salami: Iran haitafumbia macho jinai za maadui
amanda Mkuu wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) amesema Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katu haitoacha jinai za maadui zipite hivi hivi bila ya kupewa majibu makali. Brigedia Jenerali Hossein Salami alisema hayo jana Ijumaa hapa Tehran akihutubia marasimu ya kumbukumbu ya kufa shahidi Jenerali Hassan Tehrani-Moghaddam, ‘Baba wa sekta ya makombora ya Iran’…

Faili la pili la sauti ya mwandishi wa BBC: Lengo la ghasia ni kuigawa Iran
Faili la pili la sauti lililovuja la mwandishi wa Shirika la Utangazaji la Uingereza BBC limefichua wazi zaidi jinsi televisheni inayofadhiliwa na Saudia inayojiita ‘Iran International’ inavyoongoza kampeni ya kuigawa Iran vipande vipande. Ghasia zilizuka Iran wiki za hivi karibuni baada ya Bi. Mahsa Amini aliyekuwa na umri wa miaka 22 kuanguka katika kituo cha…

Sisitizo jingine la Marekani la kuunga mkono vurugu na machafuko nchini Iran
Ned Price, msemaji wa Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Marekani ameendelea kuunga mkono vurugu na machafuko nchini Iran na kukana kabisa kuhusika nchi yake katika vurugu hizo. Price amesema kuhusiana na madai ya Rais Joe Biden wa Marekani na matamshi yake ya wazi ya kuingilia masuala ya ndani ya Iran ambayo yamekabiliwa na ulegezaji…

Iran yaipa mkono wa pole Tanzania kwa vifo vya watu waliofariki katika ajali ya ndege
Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Jamhuri ya Kiislamu ametuma salamu za rambirambi kwa serikali na wananchi wa Tanzania kufuatia ajali ya ndege iliyosababisha vifo vya raia kadhaa wa nchi hiyo. Kwa mujibu wa shirika la habari la IRNA, Nasser Kan’ani amesema Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imesikitishwa na kuhuzunishwa na vifo vya…