
Leo wananchi wa Iran wanafanya maadamano ya nchi nzima kulaani shambulio la kigaidi
Wananchi wa jiji la Tehran na miji yote ya Iran, leo baada ya Sala za Ijumaa, watafanya maandamano makubwa ya nchi nzima kulaani shambulio la kigaidi lililotokea juzi Jumatano katika Haram Tukufu ya Shah Cheragh ya mjini Shiraz, kusini magharibi mwa Iran. Genge la kigaidi la ISIS limetangaza kuhusika na jinai hiyo. Kwa mujibu wa…

Shambulio la kigaidi katika Haram ya Shah Cheragh; mfano mwingine wa mradi wa kuvuruga usalama wa Iran
Ikiwa ni katika kuendeleza mradi wa maadui wa kuvuruga usalama na kuibua machafuko nchini Iran, siku ya Jumatano idadi kubwa ya wafanyaziara katika Haram takatifu ya Ahmad bin Musa (as) huko katika mji wa Shiraz waliuawa shahidi na wengine wengi kujeruhiwa kufuatia shambulio la kigaidi lililotekelezwa katika haram hiyo. Jumatano alasiri gaidi mmoja wa kundi…

Sisitizo la Iran la kutotumiwa droni zake katika vita vya Ukraine na kuwa tayari kuchunguza madai ya nchi hiyo
Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran Hossein Amir-Abdollahian amesema, Tehran iko tayari kuchunguza madai ya serikali ya Ukraine kuhusu kutumiwa na Russia ndege zisizo na rubani za Iran katika vita vya Ukraine. Amir-Abdollahian aliyasema hayo jana Jumatano baada ya mkutano wake na Waziri wa Mambo ya Nje wa Belarus Vladimir…

Iran: Uungaji mkono wa Magharibi kwa Israel ni mfano mkubwa zaidi wa ukiukaji wa haki za binadamu
Msemaji wa Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Iran amelaani shambulio la utawala ghasibu wa Israel katika mji wa Nablus katika Ukingo wa Magharibi huko Palestina inayokaliwa kwa mabavu, na kuutaja uungaji mkono usio na kikomo wa Marekani na nchi nyingine za Magharibi kwa utawala dhalimu wa Israel kuwa ni kielelezo kikubwa zaidi cha ukiukwaji…

Nyaraka nyeti zinazohusiana na Iran zimekutwa kwenye makazi ya Trump Florida
Gazeti la Washington Post limeripoti kuwa nyaraka nyeti zinazohusiana na Iran zimekutwa nyumbani kwa rais wa zamani wa Marekani Donald Trump. Tarehe 8 Agosti, maafisa ya Polisi ya Upelelezi ya Marekani FBI walivamia makazi ya Trump ya Mar- a-lago mjini Florida na kunasa maboksi 33 ya nyaraka, yakiwemo 11 yenye nyaraka nyeti za siri. Imeelezwa kuwa…

MOSSAD imeua maafisa wake sita wa intelijensia kwa tuhuma za kuwa na uhusiano na Iran
Utawala haramu wa Kizayuni wa Israel umewaua maafisa wake sita muhimu kufuatia kufeli operesheni ya shirika lake la ujasusi Mossad ya kufanya hujuma na uharibifu kwenye kituo kimoja cha viwanda mkoani Esfahan nchini Iran. Maajenti wa shirika la ujasusi la utawala wa Kizayuni Mossad walipanga kuripua kituo kimoja cha viwanda mkoani Esfahan, lakini walikamatwa na wizara ya…

IMF:Iran nchi ya 21 yenye nguvu kiuchumi duniani
Mfuko wa Fedha wa Kimataifa (IMF) umesema kuwa, Iran ni nchi ya 21 yenge nguvu kiuchumi duniani na kwamba nchi 171 duniani mwaka huu wa 2020 zimekuwa na uchumi wa kiwango cha chini ikilinganishwa na Iran. Shirika la IMF limetabiri katika ripoti yake mpya juu ya kiwango cha uzalishaji wa ndani wa nchi 192 duniani…

Vikwazo, ugaidi, vita na umwagaji damu; matokeo ya uchukuaji maamuzi ya upande mmoja
Rais Ibrahim Raisi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran adhuhuri ya jana Jumatatu aliwasili mjini New York akiuongoza ujumbe wa ngazi za juu wa Tehran kwa minajili ya kushiriki katika mkutano wa 77 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa. Akizungumza na waandishi wa habari alibainisha ratiba ya safari yake mjini New York. Rais wa…