Waziri Mkuu wa Iraq kujiuzulu iwapo mkwamo wa kisiasa utaendelea kushuhudiwa
Waziri Mkuu wa Iraq ametishia kuwa atajiuzulu wadhifa wake huo iwapo mkwamo na mgogoro wa kisiasa utaendelea kushuhudiwa nchini huo. Mustafa al-Kadhimi alitoa indhari hiyo jana Jumanne na kusisitiza kuwa, “Nitaachia ngazi kulalamikia hali ya kisiasa isiyoeleweka.” Taifa hilo la Kiarabu limekuwa katika mvutano wa kisiasa, uliopelekea kushindwa kuunda serikali tangu baada ya uchaguzi wa…
Raisi: Kuimarishwa uhusiano wa Saudi Arabia na Iran ni kwa maslahi ya usalama wa eneo
Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema ubunifu na hatua za Iraq katika kuboresha ushirikiano baina ya nchi za eneo bila uingiliaji wa madola ajinabi ni jambo ambalo limekuwa na taathira na kuongeza kuwa: “Kurekebishwa na kuimarishwa uhusiano wa Iran na Saudi Arabia ni kwa maslahi ya usalama wa eneo.” Kwa mujibu wa taarifa,…
Muqtada Sadr na machafuko ya Iraq
Jumapili ya jana tarehe 29 Agosti Iraq Jumapili ilishuhudia sokomoko na matukio ambayo kimsingi yalitabiriwa kutokea. Wimbi la machafuko hayo lilienea huku chanzo na chimbuko lake likiwa ni mwenendo wa kisiasa wa Muqtada Sadr, Kiongozi wa Harakati ya Sadr ya Iraq. Jumapili ya jana Ayatullah Hairi Marjaa Taqlidi wa Kishia ambaye anatambuliwa na wengi kama muungaji mkono wa…
Muqtada Sadr atangaza kujiuzulu siasa
Muqtada Sadr, Kiongozi wa Harakati ya Sadr ya Iraq ametangaza kujiuzulu harakati na shughuli zote za kisiasa. Uamuzi huo ambao haukutarajiwa hasa katika kipindi hiki cha mkwamo wa kisiasa nchini Iraq ambao mrengo wake unatuhumiwa kuhusika, ameuchukua baada ya taarifa muhimu iliyotolewa na Ayatullah Sayyid Kadhim Hairi. Sayyid Muqtada Sadr ametangaza kuwa, hakuna wakati ambao…
Mazungumzo ya vyama; njia ya kuikwamua Iraq katika mgogoro
Rais, Waziri Mkuu na Spika wa Bunge pamoja na vyama kadhaa vya siasa vya nchi hiyo wametoa taarifa wakisisitizia ulazima wa kukomeshwa aina yoyote ile ya mzozo na mvutano katika mitaa na barabara za nchi hiyo. Aidha wamesisitizia umuhimu wa kufanyika mazungumzo kwa ajili ya kuikwamua nchi hiyo na mgogoro wa sasa unaoikabili. Iraq imeendelea…
Iraq katika mkondo wa kushtadi zaidi mkwamo wa kisiasa
Uamuzi wa makundi na mirengo ya kisiasa ya Iraq wa kufanya mikusanyiko ya barabarani umeifanya anga ya kisiasa ya nchi hiyo kuwa tete zaidi na mkwamo wa kisiasa unaoikabili nchi hiyo kushtadi zaidi. Iraq imeendelea kushuhudia mkwamo wa kisiasa kwa miezi kumi sasa ambao chimbuko lake ni matokeo ya uchaguzi wa Bunge uliofanyika Oktoba mwaka…
Magaidi 50 wa Daesh wahamishiwa Iraq kutoka nchini Syria
Kitengo cha upashaji habari cha jeshi la Iraq kimetoa ripoti rasmi na kusema kuwa karibu wanachama 50 wa genge la kigaidi na ukufurishaji la Dashe (ISIS) wamehamishiwa mkoani Nainawa (Nineveh) Iraq kutoka katika kambi ya al Hawl ya nchini Syria. Kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa, hivi sasa kuna takriban wakazi 56,000 katika kambi ya…
Wanamichezo Wairaq wakataa kupambana na timu ya Israel katika mashindano ya Romania
Wanamichezo wawili Wairaqi wa mchezo wa tenisi wamekataa kupambana na wanamichezo kutoka utawala haramu wa Kizayuni wa Israel katika michuano ya Paralampiki inayofanyika nchini Romania. Wanamichezo wengi wanaounga mkono Palestina katika nchi za Kiislamu na Kiarabu hawautambui utawala wa Kizayuni na hawako tayari kupambana na wapinzani wao wanaowakilisha Israel katika mashindano mbalimbali ya michezo. Tovuti…