Malengo ya pamoja ya Aal-Khalifa na Israeli kuhusu safari ya Herzog mjini Manama
Isaac Herzog, mkuu wa utawala wa Kizayuni unaokalia kwa mabavu Quds Tukufu, aliwasili nchini Bahrain tarehe 4 Disemba kwa ziara rasmi ambapo alikutana na kuzungumza na Mfalme Hamad bin Issa wa nchi hiyo. Safari hiyo imefanyika kwa mwaliko rasmi wa mfalme huyo. Isaac Herzog alitangaza mapema Jumamosi kwamba alikuwa amepanga kuelekea Manama kwa mwaliko wa…
Hizbullah kuiadhibu Israeli iwapo itafanya upumbavu kuhusu mapatano ya baharini
Naibu Katibu Mkuu wa Hizbullah ya Lebanon Sheikh Naim Qassem ameonya kuwa harakati hiyo ya muqawama (mapambano ya Kiislamu) itauadhibu utawala haramu wa Israel na kuurudisha kwenye fahamu zake endapo utafanya upumbavu wowote katika suala la makubaliano ya kuweka mipaka ya baharini na Lebanon. Kiongozi huyo nambari mbili katika Hizbullah alitoa kauli hiyo Alkhamisi na…
UN: 2022, mwaka wa mauaji zaidi katika ardhi za Palestina katika miaka 16 iliyopita
Mratibu wa Misaada ya Kibinadamu wa Umoja wa Mataifa katika Maeneo Yanayokaliwa kwa Mabavu ametangaza katika ripoti yake kwamba mwaka huu wa 2022 ulikuwa mwaka wa umwagaji damu zaidi katika ardhi za Palestina katika kipindi cha miaka 16 iliyopita. Ili kufikia malengo yao ya kujipanua zaidi, Wazayuni wamekuwa wakishambulia maeneo tofauti ya Palestina na kuuawa…
Nyayo za mafia Waisraeli katika madai ya Wizara ya Sheria ya Marekani dhidi ya IRGC
Wizara ya Sheria ya Marekani imechapisha taarifa inayodai kuwa mtu mmoja kwa jina Shahram Poursafi, ambaye wizara hiyo ilimtaja kuwa mwanachama wa Jeshi la Iran la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC), alipanga kumtumia Mmarekani mmoja kumuua John Bolton na afisa mwingine wa utawala wa Donald Trump. Madhumuni ya njama hiyo imetajwa kuwa ni kulipiza kisasi…
Maandamano makubwa ya kupinga Israel nchini Uturuki
Wananchi wa Uturuki jana Ijumaa, kwa mara nyingine tena walimiminika mabarabarani katika maandamano ya kulaani ziara tata ya rais wa utawala wa Kizayuni wa Israel nchini mwao. Waturuki walioshiriki maandamano ya jana walikuwa wamebeba bendera za harakati za mapambano za Hizbullah ya Lebanon na Ansarullah ya Yemen, na vilevile picha za Shahidi Luteni Jenerali Qassem Soleimani,…
Harakati zinazotia shaka katika mkoa wa Al-Mohra nchini Yemen; Kuwasili kwa maafisa wa Kizayuni
Duru za habari za serikali iliyojiuzulu ya Yemen zimetangaza ujio wa idadi ya watu kadhaa ya maafisa wa Kizayuni katika mkoa wa kistratijia wa Al-Mohra ulioko mashariki mwa Yemen. Duru za habari za serikali iliyojiuzulu ya “Abd al-Mansour Hadi” huko Yemen zimetangaza kuwasili kwa idadi mpya ya maafisa wa utawala wa Kizayuni katika mkoa wa…
Waziri wa Mambo ya Nje wa Afrika Kusini: Hivi karibuni tutachukua hatua dhidi ya ubaguzi wa rangi wa Israel
Faraan : Waziri wa Mambo ya Nje wa Afrika Kusini alikosoa vikali utawala huo ghasibu na ubaguzi wake wa rangi dhidi ya Wapalestina. Kulingana na Fars News Agency International Group; Waziri wa Mambo ya Nje wa Afrika Kusini Nalidi Bandur katika hotuba yake mbele ya bunge aliukosoa utawala wa Kizayuni wa Israel kwa uvamizi wake…
Rais Abdelmadjid Tebboune : Morocco na Israel chanzo cha fitina nchini Algeria
Faraan : Rais wa Algeria amesema kuwa Israel na Morocco zinafanya njama ya kuibua hitilafu kati ya Ofisi ya Rais na Jeshi la Algeria na kuzusha fitna nchini humo. Kwa mujibu wa shirika la habari la Fars, Rais Abdelmadjid Tebboune wa Algeria amesema kwamba, Morocco na utawala wa Kizayuni wa Isarael ndio wanaoendesha njama za kuzusha fitina na kueneza…
- 1
- 2