
Mbunge Farah Maalim akashifiwa kwa kuvaa skafu ya Palestina bungeni
Nairobi, Kenya : Mbunge wa Kenya aliamriwa kuvua skafu ya kitamaduni ya Wapalestina aliyokuwa amevaa wakati wa shughuli za bunge, Siku ya Jumatano. Farah Maalim alisema alikuwa amevaa skafu hiyo kuonyesha alama ya mshikamano na Wapalestina huko Gaza, huku kukiwa na mzozo unaoendelea kati ya Israel na kundi la waislamu wa Palestina Hamas. Alisema Palestina…

Watu 4 wauawa katika shambulio linaloshukiwa kufanywa na al Shabab, kaskazini mwa Kenya
Watu wasiopungua wanne wameuawa na wengine kadhaa wamejeruhiwa baada ya gari lao kukanyaga bomu katika shambulio linaloshukiwa kufanywa na genge la ukufurishaji la al Shabab, huko Garisa, kaskazini mwa Kenya. Jeshi la Polisi laa Kenya limethibitisha habari hiyo na kusema kuwa, Wahandisi wa Mamlaka ya Taifa ya Barabara za Kenya ni miongoni mwa watu waliouawa…

Kiongozi wa upinzani Kenya aonya kuhusu Msikiti kutumiwa katika malumbano ya kisiasa
Kiongozi mkuu wa upinzani nchini Kenya amemuonya mwanasiasa maarufu Muislamu nchini humo kuhusu kuutumia Msikiti kama jukwaa la kisiasa. Kiongozi wa chama cha ODM na muungano wa upinzani wa Azimio Raila Odinga amemuonya Waziri wa Ulinzi Aden Duale dhidi ya kutumia Msikiti huo kama jukwaa la kisiasa. Akizungumza Ijumaa mjini Mombasa, Raila pia alimuonya Mwenyekiti…

Zaidi ya watoto milioni 3.5 wa Kenya kukosa skuli mwezi Januari kutokana na ukame
Shirika la misaada ya kibinadamu la Save the Children limetoa taarifa na kusema kuwa, zaidi ya watoto milioni 3.5 wa Kenya hawataweza kujiandikisha shuleni wakati masomo yatakapoanza mwezi Januari 2023 kutokana na ukame wa kupindukia. Katika taarifa yake ya jana Jumanne, shirika hilo limesema, utafiti wake unaoesha kuwa, ukame unazidi kuwa mbaya na watoto wengi…

Winnie Odinga: Nchi za Magharibi zimeingilia uchaguzi wa urais mwezi Agosti wa Kenya
Winnie Odinga, bintiye kiongozi wa Muungano wa Azimio, Raila Odinga, amesema kuwa nchi za Magharibi zilitumiwa kushawishi na kuyapa mwelekeo matokeo ya uchaguzi wa urais wa Agosti 9. Akizungumza katika Katika mahojiano na runinga ya Citizen, Winnie ameishutumu Marekani kwa kuingilia masuala ya kisiasa ya Kenya mara kwa mara kwa maslahi ya kibinafsi. Binti huyo…

Kundi la kwanza la wanajeshi wa Kenya latua mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo
Wanajeshi wa Kenya jana Jumamosi walitua katika mji wa Goma mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo’ ambapo walilakiwa na maafisa husika na wanajeshi wa Kongo katika eneo. Wanajeshi wa Kenya wamewasili katika mji wa Goma wakati kundi la waasi la M23 likiwa limeingia katika jimbo la Kivu Kaskazini la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, na…

Shirika la Ndege la Kenya kuwapiga kalamu marubani waliogoma
Makumi ya maelfu ya wasafiri wa ndani na nje ya nchi wameachwa katika njiapanda katika viwanja vya ndege vya Kenya, baada ya safari zao kukatizwa kutokana na mgomo wa marubani wa Shirika la Ndege la Kenya Airways (KQ). Zaidi ya wasafiri 15,000 wameathiriwa na mgomo huo uliosimamisha safari zaidi ya 53 za ndani na nje ya…

FAO : Zaidi ya watu milioni 4 wameathiriwa vibaya na ukame nchini Kenya
Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa (FAO) limetangaza kuwa, zaidi ya watu milioni 4 wameathiriwa vibaya na ukame nchini Kenya. Maelfu ya watoto wanahangaika kupata lishe huku baadhi ya wanafunzi wakilazimika kuacha shule kutokana na makali ya njaa yanayozikabili familia zao. Ripoti ya FAO inaeleza kuwa, katika Kaunti za kaskazini mashariki mwa…