
Mgombea urais wa Azimio Kenya apinga matokeo yaliyomtangaza Ruto mshindi
Raila Odinga, mgombea urais wa Kenya kwa tiketi ya Muungano wa Azimio amesema hakubaliani na matokeo ya uchaguzi wa rais yaliyotangazwa na Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka IEBC kwasababu mwenyekiti wa tume hiyo Wafula Chebukati alikiuka katiba kabla ya kumtangaza mshindi. Akizungumza na vyombo vya habari leo jioni katika mji mkuu Nairobi, Odinga ameeleza…

Ruto Rais mteule Kenya
Nairobi. Tume ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC) ya Kenya, Wafula Chebukati imemtangaza mgombea wa Kenya Kwanza, William Ruto kuwa Rais mteule wa Kenya. Ruto ambaye ni Naibu Rais wa Kenya, ameshinda uchaguzi huo uliokuwa na mchuano mkali kati yake na mgombea wa Azimio la Umoja, Raila Odinga aliyekuwa akipigiwa debe na Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta….

Tume ya Uchaguzi Kenya yakanusha madai ya kudukuliwa mfumo wake
Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka nchini Kenya (IEBC) imepuuzilia mbali madai kuwa mfumo wake wa kuendesha uchaguzi umedukuliwa, huku Wakenya wakiendelea kusubiri kwa hamu na shauku kuu matokeo rasmi ya mwisho ya uchaguzi wa rais. Akiongea na waandishi wa habari katika Ukumbi wa Bomas jijini Nairobi leo Ijumaa, Ofisa Mkuu Mtendaji wa IEBC, Marjan Hussein…

Waangalizi wa kimataifa wameridhishwa na uchaguzi Kenya
Waangalizi wa kimataifa wa uchaguzi wamefurahishwa na uchaguzi wa Kenya na sasa wanatoa wito wa ukabidhianaji madaraka kwa amani. Wakizungumza Alhamisi mjini Nairobi, waaangalizi walipongeza watu wa Kenya na tume ya uchaguzi kwa kuendesha uchaguzi huru, wa haki na wa kuaminika siku ya Jumanne. Kufikia Alhamisi, bado kulikuwa na mbio za farasi wawili kati ya…

Odinga ampiku Ruto; Wakenya waendelea kusubiri kwa hamu matokeo ya urais
Raila Odinga ambaye anagombea kiti rais katika uchaguzi mkuu nchini Kenya kwa chama cha Muungano wa Azimio la Umoja One Kenya, yupo kifua mbele katika matokeo ya muda, saa chache baada ya mpinzani wake wa karibu anayewania kwa chama cha UDA, William Ruto kuongoza katika matokeo ya awali ya zoezi hilo lililofanyika Jumanne. Kwa mujibu…

Katibu MKuu wa UN apongeza amani katika uchaguzi wa Kenya
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amewapongeza wananchi wa Kenya kwa kupiga kura kwa amani wakati wa uchaguzi mkuu wa nchi hiyo uliofanyika hapo juzi Agosti 9, 2022 Taarifa iliyotolewa na msemaji wa Katibu Mkuu Stéphane Dujarric kutoka New York Marekani imesema Katibu Mkuu anatambua kazi muhimu iliyofanywa na mamlaka ya Kenya pamoja…

Ruto aongoza katika matokeo ya awali ya uchaguzi wa rais Kenya
Mgombea wa kiti cha rais wa chama cha UDA katika uchaguzi mkuu nchini Kenya, William Ruto anaongoza katika matokeo ya muda ya zoezi hilo la kidemokrasia lililofanyika jana Jumanne. Kwa mujibu wa matokeo ya awali yaliyochapishwa kwenye tovuti ya Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka nchini humo IEBC yanaonesha kuwa, Ruto anaongoza kwa asilimia 52…

Waangalizi 18,000 wa ndani, na kimataifa kufuatilia mchakato wa uchaguzi Kenya
Waangalizi 18,000 wanatarajiwa kufuatilia uchaguzi mkuu wa Kenya utakaofanyika kesho Jumanne. Wafula Chebukati, mkuu wa Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka ya Kenya (IEBC) amesema tume hiyo ndiyo ambayo imetoa vibali kwa waangalizi hao. Serikali ya Kenya imetangaza kuwa kesho Jumanne Agosti 9 itakuwa siku ya mapumziko kitaifa ili kuwawezsha wananchi kujitokeza kwa wingi kupiga…