
Serikali Ya Kenya Yatoa Sh34 Bilioni Za Kukabiliana Na Kero Ya Uhaba Wa Mafuta
SERIKALI imetenga Sh34,446,813,295 katika bajeti ya ziada ya mwaka huu katika mpango wa kupunguza bei ya mafuta ili kukinga Wakenya kutokana na kupanda kwa bei ya mafuta. Hii ni baada ya Rais Uhuru Kenyatta Jumatatu, Aprili 5, 2022, kutia saini Mswada wa Bajeti ya Ziada uliopitishwa bungeni wiki jana. Hatua hiyo itatoa afueni kwa waendeshaji…

Punguzo la Bei Ya Data Waya Wa Sita Wa Intaneti Ukitua
Kenya imezindua waya wa sita wa kusambaza intaneti upitiao baharini, hali ambayo imeletea wananchi matumaini kuwa huenda gharama ya kununua data ya simu ikapungua huku kasi ya intaneti ikiongezeka siku za hivi karibuni. Kuzinduliwa kwa waya unaouanganisha Pakistan, ukanda wa Afrika Mashariki na bara Uropa (Peace) Jumanne, kunajiri wakati ambao uchumi wa intaneti nchini unakua…

TUSIJE TUKASAHAU: Vijana Waliojisajili Kidijitali Kwa Mpango Wa Kazi Mtaani Hawajaanza Kazi
MNAMO Oktoba 20, 2021 Rais Uhuru Kenyatta aliamuru Hazina ya Kitaifa kutenga Sh10 billion za kufadhili awamu ya tatu ya Mpango wa Kazi Mtaani. “Naamuru Hazina ya Kitaifa kutoa Sh10 bilioni za kugharamia awamu ya tatu ya Mpango wa Kazi Mtaani. Mpango huo ambao unalenga kufaidi zaidi ya vijana 200,000 utatekelezwa katika kaunti zote 47…

Usitumie Ikulu kama Jukwaa La Kueneza Propaganda; DP Ruto amrushia Rais Uhuru Makombora
William Ruto alisema amekubali kwamba Rais Uhuru Kenyatta hatampigia debe licha ya kumuunga mkono katika chaguzi mbili.Alimwonya kiongozi wa taifa dhidi ya kutumia Ikulu kama njia ya kueneza propaganda na ujumbe wa mgawanyiko wa kikabila Naibu Rais alimkumbusha Uhuru kwamba alisimama upande wake wakati wengi wa wale anaowaita ‘marafiki’ sasa, walikuwa maadui zake. Katika ziara…

Kenya yawawinda wanaoeneza chuki kuelekea uchaguzi mkuu wa Agosti 9
Tume ya Uwiano na Utangamano wa Kitaifa ya Kenya (NCIC), inachunguza watu 51 kwa tuhuma za kusambaza matamshi ya chuki huku kaunti sita zikikihofiwa kukumbwa na vurugu za kisiasa katika kipindi hiki nyeti cha kampeni kali za kuwapigia debe wanasia wanaowania kiti cha rais wa nchi hiyo. Mwenyekiti wa NCIC, Samuel Kobia, amesema watu 36…

Raila Odinga: Sitamwacha Uhuru Kenyatta iwapo nitashinda uchaguzi wa rais wa Agosti 9
Kiongozi wa chama cha ODM, Raila Odinga, amesema kuwa hatamwacha Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya iwapo atashinda uchaguzi wa Agosti 9, 2022. Raila amesema kuwa Rais Kenyatta amekuwa nguzo muhimu katika utulivu wa taifa na uchumi na kwamba yeyote atakayeshinda hastahili kumtelekeza. Amesema iwapo atashinda uchaguzi ujao ataendeleza uhusiano wake na Rais Uhuru Kenyatta na…

Kenya miongoni mwa nchi zitakazoanza kutengeneza chanjo za Covid-19 kwa teknolojia ya mNRA
Shirika la Afya Duniani (WHO) limetangaza kuwa, nchi sita za Afrika zimechaguliwa kuanza utengenezaji wao wa chanjo za Covid-19 kwa kutumia teknolojia ya mfumo wa mRNA. Kenya, Afrika Kusini, Nigeria, Senegal, Misri na Tunisia zimechaguliwa kuwa nchi za kwanza kupokea teknolojia ya mRNA kutoka kituo Shirika la Afya Duniani (WHO) cha kimataifa, katika bara hilo…

Mwanazuoni mkubwa wa Kiislamu Afrika, Sheikh Abdillahi Nassir, aaga dunia
Sheikh Abdillahi Nassir Juma Bhalo, msomi maarufu wa Kiislamu barani Afrika na hasa Afrika Mashariki ameaga dunia mapema leo Mombasa, Kenya. Umma wa Kiislamu umetumbikia katika majonzi makubwa kufuatia kuaga dunia Sheikh Abdillahi Nassir, ambaye alitumia umri wake wote uliojaa baraka kuhudumia Uislamu na Waislamu hususan wa kanda ya Mashariki na katikati mwa Afrika Sheikh…